WAMANG'ATI/WADATOOGA NI HATARI,WATAMBUE. - waleo blog

Breaking

Sunday 26 January 2020

WAMANG'ATI/WADATOOGA NI HATARI,WATAMBUE.


#UTALII WA NDANI

Wadatooga (pia huitwa Wamang'ati. ni kabila la watu wa Kiniloti nchini Tanzania wanaishi hasa katika mikoa ya ManyaraMaraArusha na Singida.

Lugha yao ni Kidatooga, ingawa lahaja zake zinatofautiana kiasi kwa kufanya maelewano kuwa magumu.
Kuna  makundi saba ya Wadatonga.
·         Wabajuta
·         Gisamjanga (Kisamajeng, Gisamjang)
·         Wabarabayiiga (Barabaig, Barabayga, Barabaik, Barbaig)
·         Waasimjeeg (Tsimajeega, Isimijeega)
·         Warootigaanga (Rotigenga, Rotigeenga)
·         Waburaadiiga (Buradiga, Bureadiga)
·         Wabianjiida (Biyanjiida, Utatu)


NDOA ZA KIDATOOGA
Katika  makala yetu, na leo tutaangazia suala zima la ndoa katika jamii hii ambayo ipo katika hatari ya kotoweka kutokana na wengi wao kumezwa na kabila la wairaq na wengine kutawanyika nchi nzima na kupelekea hatari ya kusahau utamaduni wao kabisa.


Kuna aina tatu ambazo hufuatwa kwenye ndoa katika jamii ya wadatooga

Kutumia mshenga na kupata ridhaa ya wazazi

Kukubaliana na binti na kumtorosha bila ridhaa ya wazazi
"Kumteka" binti bila ridhaa yake wala wazazi
Mpaka kufikia uamuzi wa kuoa, mara nyingi kijana amekuwa amemchunguza binti kwa muda wa kutosha ikiwa ni pamoja na kujua familia anayotoka hasa kuzingatia uchapa kazi, kutokuwa mchawi na pia utajiri wa ng`ombe kwani binti wa kidatooga anapoolewa hupewa zawadi za ng`ombe.
Lakini jambo la kushangaza tofauti na jamii zingine ni kuwa mahari huweza kuwa hata bunda la tumbako, asali na ndama (mweusi asiye na mabaka wala mawaa) kutokana na aina au style uliyotumia kutaka kuoa.
Jambo la tofauti ni kuwa sherehe za harusi za kidatooga huhudhuriwa na wanawake tu hata bwana harusi hatakiwi kuwa maeneo ya karibu, na hazina gharama bali wanawake huimba nyimbo zilizojaa mambo (mafunzo) kwa bibi harusi (kama kitchen Party vile)

Kutumia mshenga na kupata ridhaa ya wazazi

Unaweza kuongea "direct" na kukubaliana na baba wa binti au kumtuma mshenga ambaye anaweza kuwa baba yako na kama hakuna undugu wowote na pia kama utafikia vigezo taratibu za harusi huanza. Ijulikane kuwa binti anaweza kuchumbiwa na watu hata zaidi ya 10 na wote "hushindanishwa" na kupatikana anayefaa. Wazazi hutumia muda hata wa zaidi ya mwaka 1 kuchunguza familia ya anaye "propose" na mchakato mzima wa kuchuja hao "wagombea jimbo" huwa wazi na mnajifahamu kabisa na hata matokeo huwekwa kwa uwazi.
Vigezo vinavyotumiwa ni pamoja na tabia za familia, kama wanang`ombe au la, na kama hawana ni kwa nini? Ifahamike kuwa kwa Wadatooga unaweza kuoa hata kama hauna ng`ombe lakini kutokuwa nao si "excuse" kabisa kwani unaruhusiwa kuiba ng`ombe hasa kutoka kwa makabila mengine hasa wanyiramba na wanyaturu. Wadatoga huamini kuwa ni jambo la ushujaa kama mwanaume akifa akiwa katika harakati za kuiba ng`ombe au akifa kwa ajili ya mwanamke!
Kwa kuwa wazazi wameridhia mahari huweza kuwa tumbaku au asali au ndama mweusi kabisa asiye na madoa wala mabaka na awe hajapandwa. Na siku ya harusi mama wa binti huwekewa mafuta ya siagi kichwani kama ishara ya heshima na ufahari na binti kwa kuwa amewapa wazazi wake heshima hupewa zawadi ya ng`ombe na wazazi wake, mama hupewa zawadi ya damu iliyokaangwa na mafuta na kupeleka nyumbani kwake!
Kukubaliana na binti na kumtorosha bila ridhaa ya wazazi
Hapa unakubaliana na binti na kisha kimya kimya unamtorosha na kisha baadaye taarifa hupelekwa kwa wazazi kuwa binti yao ameshaolewa. Kwa kuwa haujapata ridhaa ya wazazi wa binti hapa lazima mahari ikutoke lakini haizidi ng`ombe mmoja lakini pia hatapewa zawadi ya ng`ombe na wazazi wake. Kwa kuwa umemshawishi akukubali mara zote lazima utakuwa umem"saundisha" kwa kumuahidi kumpa ng`ombe ili akubali kutoroka hivyo lazima utoe ng`ombe mtu mzima.
Njia hii hutumiwa mara nyingi hasa pale unapopeleka posa na kuonekana kuwa uwezekano wa kushinda "tender" ni mdogo lakini "mnapendana" yaani hii huwa plan B! na siku ya harusi mama wa binti hawezi kuhudhuria!
Kumteka" binti bila ridhaa yake wala wazazi
Ukiona njia zote mbili za juu hazina mafanikio yaani uwezekano wazazi wa binti kukukubali ni mdogo na pia "saundi" zako hazieleweki, unaandaa vijana wenzako ambao humteka binti na kumwambia wazi nia yao kuwa "tunataka kukuoa" na mara nyingi hutekwa jioni na safari ya kuelekea ukweni huanza.
Mara nyingi njia hii hutumiwa kama unautajiri mkubwa wa ng`ombe kwani ili akukubali ni lazima utampa ng`ombe wengi pengine hata 40 na hata anapokubali anakuwa chini ya ulinzi mpaka atakapojifungua. Wazazi hupewa taarifa na kama kawaida kunafaini na ukishailipa taratibu za harusi huendelea.
katika hatua zote hizo, lazima wakutoke ng`ombe wasiopungua watano ili huyo binti akifika kwenu (kwako) awe mkeo mazima. Unampa ng`ombe ili afanye haya mambo
Ili avae "Hanang`wenda" yaani sketi ya ngozi kama ishara ya pete
Anapofika mlangoni ili aingie ndani
Ili ale chakula
Usiku ili avue hanang`wenda
Ili akukubalie kula "chakula cha usiku"
Jambo la kushangaza ni kuwa hawa ng`ombe wooooote anaopewa mwanamke japo ni wake lakini haruhusiwi kuwauza wala kuwatumia kwa matumizi yoyote yale bila idhini ya mumewe na hata mumewe pia hawezi kuwatumia bila ridhaa ya mkewe. Hawa ng`ombe huwahifadhi/kuwatunza kwa ajili ya kuwarithisha watoto wake wa kiume, ikumbukwe kuwa wadatooga huwa na ndoa za mitaala yaani ya mke zaidi ya mmoja hivyo kila mwanamke huhakikisha wanawe wanapata urithi mkubwa.
Tofauti ya umri huwa si tatizo hata kama mwanaume anaumri mdogo kuliko mke na pia kaka zako au wanarika wenzako "ratta" wanahaki ya kutembea na mkewe na hautakiwi kuonesha wivu wowote. Kama kaka yako amekuzidi umri na akiwa amekubaliana na mke wako anaweza kukutaarifu kuwa leo anakuja kulala na mkeo hivyo umpishe na kama ni mdogo wake yampasa kukubaliana na "shemeji" ila asikuoneshe kuwa mnashare na anatkiwa kukuheshimu. Sipati picha kama hii ingekuwa inaruhusiwa katika jamii zingine.

Top of Form
Haya ni machache sana kuhusu Wadatooga mengi  yanafuata.Kikubwa tu usisahau kushare, kulike,kufollow ,maoni na kutukoment kwa  tafakari  zako  juu ya hiki tukifanyacho.

No comments:

Post a Comment

Pages