#KILIMO
KILIMO BORA CHA MIWA
: Kilimo cha miwa ni kilimo chenye tija kwa mkulima, kilimo hiki kinaweza
kufanywa na mtu yeyote yule aidha awe ameajieliwa au laaa!. Jambo la msingi ni
kuhakikisha anajitoa kikamilifu katika kuhakikisha unawekeza akili yako
katika kulima kilimo hiki.
Kuna aina kuu 2 za
miwa katika mbegu za miwa zilizo shamiri sana ambazo ni:
1.
Bungala
Unachotakiwa kufanya
katika kulima kilimo hiki ni, Kwanza kabisa tafuta ekari moja ya shamba kisha
anza maandalizi lakini zingatia kupuguza matumizi makubwa ya pesa kadri
iwezakanavyo yaani kwa shughuli nyinginezo ambazo unaweza kuzifanya mwenyewe ni
vyema ukazifanya ili kupunguza matumizi makubwa ya pesa mfano kulima, kupiga
dawa, kupalia n.k
Tafuta mbegu ya miwa
ya Bungala miwa hii ni laini sana na ni rahisi kuichana kwa kutumia meno, baada
ya kupata miwa hii kata vipande vipande vya pingili tatu tatu. Kumbuka kwamba
miwa ni rahisi sana kushambuliwa na mchwa pale tu inapokuwa imepandwa.
Ili kuzuia isiliwe na
mchwa nenda katika maduka ya kilimo na ununue moja wapo ya madawa yafuatayo:-
1.
TAP 4% GR Tumia gram
100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji kisha nyunyizia katika mashina ya
miwa.
2.
Taniprid 25 WG. Tumia
gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji au pia unaweza kuweka kijiko
kimoja cha chai katika kila shina.
3.
Imida Gold Mls 20 kwa
lita 20 za maji na unyunyizie shinani.
4.
Gammalin 20. Tumia gram
100 kwa lita takribani 20 za maji. Na unyunyizie katika vipande vya miwa au
chovya vipande vya miwa katika maji hayo yaliyo na Gammalin 20 na ndipo uende
ukavipande shambani kwako.
5.
Gladiator FT.
6.
Stom
Mambo yakufanya:
Zingatia kama utatumia
aidha Gladiator au Gammalin au Stom, chukua ndoo ya maji ya lita 20 kisha
uichanganye na dawa uliyoinunua kisha chukua kipande cha muwa na kukizamisha
ndani ya maji hayo na baadae uende kuipanda shambani kwako, hivyo uewezekano wa
miwa yako yote kuote utakuwa ni mkubwa sana maana shida kubwa ni mchwa na hapo
tayari utakuwa umeidhibiti.
UPANDAJI WA MIWA
Hakikisha unapokuwa
unapanda miwa yako acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mche na mche pia
hakikisha una acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mstari na mstari. Kumbuka
awali tulisema katakata muwa wako kupata vipande vilivyo na vipingili vitatu
vitatu, hivyo sasa unapokuwa unapanda miwa hii hakikisha hizo pingili zote 3
zimezama ndani ya ardhi na kipande kidogo tu ndio kibakie juu ya uso wa ardhi
na mche wako huo unapoutumbukiza kwenye ardhi uwe umelala wastani wa nyuzi 30.
Zile pingili katika
muwa wako kumbuka ndipo sehemu hasa miwa inamokuwa inachipuka na kuota. Mantiki
ya kuacha nafasi kubwa kati ya mche na mche ni kwa sababu hilo shina lako moja
ulilolipanda linaweza likachipua vijimiwa vingine zaidi hata ya ishirini kama
ukiliacha shina liendelee kuzaa tu kwa kadri linavyotaka na hatimaye shamba
lako litakuwa msitu hata usiopitika.
Lakini kibaya zaidi ni
kwamba miwa yako itakosa afya njema na mwisho wa siku miwa yako haitakuwa bora
hata bei haitakuwa nzuri pindi utakapoamua au wakati wa kuuza utakapofika.
Hivyo unashauriwa kuacha miwa kati ya tano mpaka kumi lakini mfano ukiacha miwa
mitano katika shina moja ni dhairi hewa na mwanga vitakuwa vya kutosha shambani
lakini hata chakula na virutubisho vingine kwa miwa hiyo vitakuwa lukuki na sio
vya kung’ang’aniana hivyo mwisho wa siku utapata miwa mirefu na minene ambayo
sokoni itakuwa na mvuto mkubwa kwa wateja.
Mfano chukulia kwamba
umelima ploti ndogo tu ya upana mita 50 kwa urefu mita 70, kumbukumbu namna ya
upandaji miwa kama tulivyozungumza hapo awali umbali wa mita moja moja kwa kila
shina. Hivyo kwa ploti ya shamba hili utakuwa na miche au mashina uliyopanda
kiasi cha 70×50=3500 (mashina elfu tatu na mia tano) sasa chukulia kwa hesabu
rahisi kwamba kila shina umeruhusu miwa mitano tu ndio ikuwe pale maana yake
kwa mashina 3500 utazidisha mara 5 ambapo itakuwa 3500×5= 17,500 hiyo ndio
itakuwa jumla ya miwa itakayovunwa shambani.
Kwa tafiti
zilizofanywa zinaonesha kama hautaki shida na unahitaji pesa ya haraka haraka
sana huko huko shamba, basi unaweza ukajumlisha miwa yako kwa bei ya chini sana
yaani tukadilie vile kwamba tunahitaji pesa ya haraka so tuuze muwa mmoja kwa
bei ya jumla ya 300 hivyo jumla ya pesa utakayoipata itakuwa 17,500 × 300 =
5,250,000 (milioni tano laki mbili na nusu). Hiyo ni pesa ya haraka haraka huko
huko shambani .
Ila kama ukiweza
kusogea zaidi na kuuza kwa faida maana kama umeweza kupigana mpaka kuweza
kuikuza ni dhairi kwamba unastahili kupata faida iliyo njema kwako hivyo ni
muhimu kuangalia masoko yamekaaje pande zote za miji, ila kama utaweza
kuifikisha Dar es Salaam ambako kiuhalisia soko lake ni kubwa sana .
Kama ukienda Kariakoo
bei ya rejareja kwa muwa aina ya bungala wenye wastani wa urefu mita moja na
robo bei yake ni 5,000 lakini ukienda mtaani kwa muwa huo huo aina ya bungala
mfupi kidogo bei yake inakwenda mpaka 3,500 hivyo chukulia kwamba umeweza
kufikisha Dar es Salaam huo mzigo wako wa miwa, hivyo mapato yako kama utaamua uuze
kwa bei ya jumla ya 1,500 kwa kila muwa hivyo kiasi cha fedha utakachokipata
kitakuwa ni sawa na idadi ya miwa yako zidisha bei ya kujumlishia yaani
ingekuwa 17,500 × 1,500= 26,250,000 hii ni pesa utayoipata kwa halali kabisa
wala haujamzulumu mtu.
Hapo umelima ploti
ndogo tu, sasa chukua pengine umelima ekari moja na kwa shamba la miwa ekari
moja kiwango cha chini kabisa cha wewe kuvuma miwa yako ni jumla ya miwa
24,500. Sasa chukulia kama umeweza kuipeleka Dar es Salaam maana yake utapata
jumla ya 24,500 × 1,500= 36,750,000. Sasa mfano ndo ukalima ekari 4 hadi 5 hapo
ni hakika unatoka katika kundi la uchumi wa chini na kuingia katika uchumi wa
kati. Jamani bado hatujachelewa kungali bado fursa ziko kinachohitajika hapa ni
kuthubutu tu, Mungu akubariki unapoyatafari haya lakini pia pindi ukifanikiwa
usimsahau Mungu maana yeye ndiye nguzo ya mafanikio yako yote.
No comments:
Post a Comment