#AFYA
“Tucheke kidogo, kabla ya kuingia katika makala haya.Haha hahaaaa!!yaani hehe heheeeee!...KUNGUNI bwanaaaa! Hutusaidia sisi wanafunzi tuishio kwenye mabweni yetu, ambao pia ni wavivu wa kuamka usiku kusoma.. ”Binafsi naona hii ni faida kung’atwa na kunguni’’.
Kufikia
katikati ya karne ya 20, ilionekana kwamba wanadamu wamefaulu kuwadhibiti
kunguni. Watu fulani walifahamu kunguni kupitia tu wimbo wa zamani wa
Kiingereza ulioimbwa na watoto wa shule za nasari (au chekechea) uliosema:
“Usiwaache kunguni wakuume.” Hata hivyo, katika miaka ya 1970, nchi nyingi
ziliamua kupiga marufuku matumizi ya dawa ya DDT—iliyokuwa dawa kuu ya kuua
kunguni—kwa kuwa ilikuwa yenye sumu na iliharibu mazingira.
Hata
hivyo, kemikali nyingine zilipotumiwa ilionekana kwamba kunguni walikuwa sugu
na hazikuwaua. Pia watu walianza kusafiri mara nyingi zaidi na bila kujua
walihama pamoja nao. Matokeo yakawaje? Ripoti moja ya mwaka wa 2012 kuhusu
kuwadhibiti wadudu hao inasema: “Katika miaka 12 ambayo imepita kunguni
wameanza kuonekana tena nchini Marekani, Kanada, Mashariki ya Kati, nchi kadhaa
za Ulaya, Australia, na katika sehemu fulani za Afrika.”
Huko
Moscow, Urusi, katika mwaka mmoja hivi karibuni, ripoti za kutokea kwa kunguni
ziliongezeka mara kumi kuliko ilivyokuwa hapo awali. Wakati huohuo, upande ule
mwingine wa ulimwengu, huko Australia, kumekuwa na ongezeko la kunguni tangu
mwaka wa 1999!
Watu
fulani hubeba kunguni bila kujua wanapoenda dukani, kwenye kumbi za sinema, au
hotelini. “Upende usipende utabeba kunguni,” anasema meneja fulani wa hoteli
nchini Marekani. “Maadamu hoteli inapata wateja lazima kunguni wataendelea
kuwapo.” Kwa nini ni vigumu kiasi hicho kuwamaliza kunguni? Unaweza
kujilindaje? Kunguni wanapovamia nyumba yako, unaweza kuchukua hatua gani
zinazofaa ili kuwaondoa na kuwazuia wasirudi tena?
Wadudu Wasiokufa kwa Urahisi
Kwa kuwa wadudu hao ni
wadogo kama mbegu ya tofaa na wana mwili bapa, kunguni wanaweza kujificha
mahali popote pale. Wanaweza kujificha katika godoro lako, fanicha zako, sehemu
ya ukutani ya kuunganishia vitu vya umeme, au hata kwenye simu yako. Kwa
kawaida kunguni hupenda kujificha mita tatu hadi sita kutoka kwenye vitanda na
maeneo ya kuketi. Kwa nini? Ili wawe karibu na chakula chao, yaani, wewe
msomaji na mimi mwandishi.
Mara
nyingi, kunguni huwauma watu wanapolala. Hata hivyo, watu wengi hawahisi
wanapoumwa kwa sababu mdudu huyo humdunga mtu kitu kinachogandisha
kinachomwezesha kuendelea kula kwa dakika kumi hivi bila kukatizwa. Na ingawa
kunguni wanaweza kula kila juma, imesemekana kwamba wanaweza kuendelea kuishi
bila kula kwa miezi mingi.
Tofauti
na mbu na wadudu wengine, inaonekana kwamba kunguni hawaenezi magonjwa ya
kuambukiza. Hata hivyo, wanapomuuma mtu wanatokeza mwasho na baadaye sehemu
hiyo inavimba, na watu wengi huathiriwa kihisia. Watu walioumwa na kunguni
wanaweza kupoteza usingizi, kuaibika, na hata kufikiri kwamba kunguni
amewauma muda mrefu baada ya wadudu hao kutoweka. Jarida moja nchini Sierra
Leone linasema kuwa kunguni “ni wasumbufu sana na wanawakosesha watu usingizi”
na linaonya kuhusu “aibu inayohusianishwa na kunguni.”
Kuwadhibiti Kunguni
Kunguni
wanaweza kumsumbua mtu yeyote. Ni rahisi kuwadhibiti ukitambua mapema kwamba
wapo. Kwa hiyo, jifunze kutambua ishara za kwamba wapo nyumbani na unaposafiri.
Chunguza fanicha zako na vitu vingine vya mbao pamoja na mizigo, uone ikiwa
kuna mayai madogo yanayofanana na mbegu ndogo nyeusi au alama za damu. Tumia
tochi unapowatafuta kunguni ili uweze kuwaona.
Usiruhusu
kunguni wawe na sehemu nyingi za kujificha. Ziba nyufa zote ukutani na kwenye
viunzi vya milango. Ingawa kunguni hawaletwi na uchafu, itakuwa rahisi zaidi
kuwatambua na kuwadhibiti ikiwa unasafisha nyumba kwa ukawaida na kupunguza
vitu vilivyorundamana. Ukiwa hotelini, unaweza kupunguza uwezekano wa kubeba
kunguni kwa kuepuka kuweka masanduku yako sakafuni na kitandani.
Kunguni wanapovamia nyumba yako
Ukipata
kunguni nyumbani au hotelini, huenda ukawa na wasiwasi au hata ukaaibika. Saad
na mke wake waliumwa na kunguni walipokuwa likizoni. Saad anasema: “Tuliaibika
sana. Tulijiuliza tutawaambia nini watu wa familia na marafiki tutakapofika
nyumbani? Je, wakati wowote wanapojikuna au kupatwa na mwasho wa ngozi
wangejiambia ni kwa sababu walitutembelea?” Hata ingawa ni kawaida kuwa na
maoni kama hayo, usiache aibu ikuzuie kutafuta msaada. Wizara ya afya ya mwili
na akili ya New york city inatoa uhakikisho huu: “Ni vigumu, lakini inawezekana
kuwaangamiza kunguni.”
Chunguza uone kama
kuna kunguni kisha uchukue hatua za kuwazuia wasijifiche nyumbani kwako
Hata
hivyo, usifikiri kwamba ni rahisi kuwamaliza kunguni. Kunguni wakivamia nyumba
yako, unaweza kupata msaada kutoka kwa mtaalamu wa kuwadhibiti wadudu
wasumbufu. Ingawa kemikali zilizotajwa awali hazitumiwi tena, wataalamu hao
hutumia mbinu kadhaa zinazofaa ili kuwaangamiza kunguni. Din M. Miller,
mtaalamu wa wadudu anasema hivi pia: “Kuwadhibiti kunguni kunahitaji
ushirikiano mkubwa sana kati ya wakaaji wa nyumba, wamiliki wa nyumba yenyewe,
na kampuni ya kuwadhibiti wadudu wasumbufu.” Kwa kufuata mwelekezo wa mtaalamu
na kuchukua tahadhari zinazohitajika, unaweza kutimiza sehemu yako na
‘kutowaacha kunguni wakuume’!
Wataalamu wa wadudu wanasema kwamba kunguni
hula damu ya wanadamu na wanyama wengine..
Maji ya moto nayo hupunguza kasi ya kunguni.Chemsha
maji hayo na uyamwagie mazalia yao.
Kwa huduma ya kuua wadudu wadogo wa nyumbani na makazini, tupigie simu namba 0782080716 kwa mkoa wa morogoro tu
No comments:
Post a Comment