#UTALII
Nyangumi ni wanyama wa bahari, na pengine wa maji
matamu,
katika oda Cetacea wanaofanana
na samaki, lakini ni mamalia: kwa hivyo hawatagi mayai kama samaki bali
huzaa watoto kama mamalia wote na huwanyonyesha.
Oda yao ina spishi 80 hivi. Spishi
ndogo huitwa pomboo kwa kawaida na
spishi kadhaa za pomboo huishi kwenye maji matamu ya mito mikubwa kama Ganges au Amazonas.
Mwili wote unalingana na
maisha ya majini. Nyangumi wanaotupwa kwenye nchi
kavu wanakufa
haraka: wanakauka, uzito wa mwili
unagandamiza mapafu kwa sababu
wanakosa ueleaji wa maji.
Hata hivyo muundo wa
mwili ni sawa na mamalia wengine:
·
wanapumua kwa kutumia mapafu;
kutegemeana na spishi zinaweza kuzama na kukaa chini ya maji kuanzia dakika kadhaa hadi masaa
mawili.
·
Nyangumi huwa na damu
moto yaani
wanaweza kutunza halijoto ya wastani mwilini, tofauti na
samaki wanaobadilika halijoto ya mwili kulingana na halijoto ya mazingira.
·
Wanazaa watoto waliokamilika tayari na
kuwanyonyesha maziwa yenye mafuta mengi kwa
kutumia viwele vyao. Mimba hukua mwilini
mwa mama hadi kuwa mnyama
kamili jinsi ilivyo kwa mamalia wengi.
Spishi nyingi za nyangumi
ni kubwa sana. Nyangumi buluu (Blue
whale)
anaweza kufikia uzito wa tani 200 na urefu wa mita 33.
·
wale wanaowinda samaki au wanyama wakubwa
wengine wa bahari wana meno ya kawaida.
·
wale wanaokula planktoni (viumbe
hai vidogo
sana baharini) hawana meno, bali mifupa ya kinywani ambao si mifupa ya
kweli, ila inaundwa na kitu kinachofanana na kucha za vidole. Mifupa hiyo inakaa kama
meno ya chanuo na inafanya kazi
ya filta; nyangumi huyo
anafungua mdomo na kujaza nafasi
maji pamoja na yote yaliyomo kama uduvi wadogo sana; ulimi unasukuma maji
kupitia chanua ya mifupa ya kinywani na windo unabaki ndani kama
chakula.
Nyangumi ni jina la jumla
la mamalia wa majini wa oda ya Cetacea. Neno nyangumi wakati fulani humaanisha
wanyama wote wa oda ya Cetacea, lakini katika lugha ya kawaida huwaacha wanyama
wa familia ya Delphinoidea, kama vile pomboo.
Spishi ndogo hizi huwa
ndani ya oda ndogo ya Odontoceti (nyangumi wenye
meno), ambayo hujumuisha nyangumi kadhaa.
Oda nyingine ndogo ya
Cetacea ni Mysticeti, ambayo hujumuisha
nyangumi wa bluu, ambaye ndiyo mnyama mkubwa kuliko wote aliyeripotiwa kuishi,
nyangumi mwenye nundu, na wanyama wengine wanaokula kutoka kwenye maji ya
baharini kutumia michirizi mirefu iliyopo
badala ya meno, ambayo ndiyo walikopatia jina lao.
Kama mamalia wengine,
nyangumi hutumia mapafu kupumua, wana damu joto, wananyonyesha watoto wao kwa
kutumia viwele, wana vinyweleo, japo kidogo sana.
Mwili wa nyangumi umeungana.
Miguu ya mbele, imekaa muundo wa kasia. Mwishoni mwa mkia kuna tiara, au pezi
la mkia, ambalo lina saidia kwenye mwendo hasa wima tofauti na kwa mwendo mlalo
wa samaki. Japokuwa nyangumi hawana miguu ya nyuma, lakini baadhi yao wanamiguu
isiyokamilika; iliyojificha ndani ya miili yao. Spishi nyingi za nyangumi wana
pezi migongoni mwao inayojulikana kama pezi la mgongoni.
Chini ya ngozi yao wana
utando wa mafuta. Mafuta haya ni kwaajili ya kuhifadhi nishati na kuzuia
upotevu wa joto. Nyanguumi pia wana moyo wenye vyumba vinne. Nao pia wana uti
wa mgongo japo pingili za shingoni pia zimeungana kwaajili ya kuimarisha uwezo
wa kuogelea na kuongeza uhuru wa kufanya hivyo. Wanao pia mfupa wa nyonga
usiokuwa na kazi maaluumu.
Nyangumi wanapumua
kutumia matundu ya hewa, yaliyo juu ya vichwa vyao ili kuwawezesha kupumua huku
wakiwa wamezama majini. Nyangumi wa baleen wanayo mawili; na nyangumi wenye
meno wana moja tu. Kupumua hujumuisha kutoa maji zaidi kutoka kwenye matundu
hayo ya hewa na, na kuunda bubujiko la maji. Bubujiko hizi huwa na maumbo
mbalimbali na wakati mwingine hutumika kuwatofautisha na hatimaye kuwatambua
baadhi ya nyangumi.
Nyangumi wa bluu ndiye
mamalia mkubwa zaidi aliyepata kuishi, na pia mnyama mkubwa, kufikia mpaka mita
35 kwa urefu na uzito wa tani 150.
Nyangumi kwa wastani
wanaishi miaka 40 mpaka 90, kulingana na aina zao na mara chache hufanikiwa
kiushi zaidi ya karne moja. Hivi karibuni kipande cha kamba kilichokuwa
kinatumiwa na wavuvi wa nyangumi wa karne
ya 19,
kilipatikana kwa nyangumi huko Alaska, na kuonesha kuwa
nyangumi yule alikuwa na umri kati ya miaka 115 na 130. kwa kutumia mbinu
ya kupima umri kwa kuangalia kiwango cha aspatiki asidi kwenye macho ya
nyangumi, pamoja na kipande cha chusa, vilionesha umri wa miaka 211 kwa
nyangumi mmoja, na kuwafanya nyangumi pia kuwa wanyama wanaoishi kwa muda mrefu
zaidi. Mkia wa nyangumi unaweza
kuwa pia kama alama ya kuwatambua, kama ilivyo kwa nyangumi wenye nundu mgongoni.
Meno ya nyangumi wenye
meno kama vile nyangumi aitwaye sperm, wana seli za sementamu zilizo juu ya
seli za dentaini. Tofauti na binadamu wenye meno yenye kiasi kikubwa cha
enameli kwenye sehemu ya nje ya jino, nyangumi wana sementamu nje ya fidhi. Ni
kwa nyangumi wakubwa pekee ambao enameli yao huonesha pale ambapo sementamu
ilipotoka.
Nyangumi huonwa kama ni
wawindaji mara zote, lakini chakula chao ni kuanzia plankitoni mpaka samaki
wakubwa kabisa, na wakati mwingine wanyama wengine wa baharini, hata nyangumi
wengine. Nyangumi hasa wale wenye nundu mgongoni na wale wa bluu wanakula tu
kwenye maji ya aktiki, ambapo humeza vitoweo vyao pamoja na maji mengi, na
baadae kutoa maji kupitia baleen huku wakibakiza vitoweo vyao kinywani.
Nyangumi hawanywi maji ya
baharini na badala yake hutengeneza maji kutoka kwenye chakula chao kwa
metabolizimu ya mafuta.
Nyangumi wengi huonesha
tabia nyingi za majini kama vile kujitokeza juu na kupigiza mkia.
Kulingana na mazingira
yao (tofauti na na wanyama wengine), nyangumi hupumua kwa hiari yao, wanaamua
ni wakati gani wa kupumua. Mamalia wote hulala lakini nyangumi hawawezi kulala
kwa muda mrefu sababu wanaweza zama majini na kufa. Husemekana ni nusu tu ya
ubongo wa nyangumi hulala na sehemu nyingine hufanyakazi, hivyo nyangumi huwa halali
moja kwa moja lakini hupumzika vya kutosha. Mara nyingi nyangumi hulala huku
jicho moja tu likiwa limefungwa. Baadhi ya nyangumi huwasiliana kwa sauti za
kimuziki, zikijulikana kama nyimbo za nyangumi. Sauti hizi zaweza kuwa kubwa
sana kutegemeana na spishi zao. Nyangumi waitwao sperm husikika wakitoa sauti
za kugonga gonga tu, kwasababu wao wana meno na hutoa pia mwangwi unaoweza
kusikika kwa maili nyingi.
Nyangumi jike huzaa ndama
mmoja tu. Muda wa kumkuza ndama huyo ni zaidi ya mwaka mmoja kwa spishi nyingi
na hujumuisha uhusiano mkubwa kati ya mama na ndama. Nyangumi huwa tayari kuzaa
wakiwa na miaka saba mpaka kumi. Mtindo huu huruhusu watoto wachache tu lakini
wakiwa na uwezo mkubwa wa kuishi.
Viungo vya uzazi vya
nyangumi huzama na kujificha ndani ya nafasi za mwili wakati wa kuogelea,
kuongeza mwendo kasi na kuzuia majeraha. Nyangumi wengi hawana wenzi wa aina
moja; na majike wengi hubadilisha madume kadhaa kila msimu. Watoto wa nyangumi
huzaliwa kwa kutoa mkia kwanza utaratibu unaopunguza hatari ya kufa maji.
Nyangumi pia hujulikana
kwa uwezo wao wa kufundisha na kujifunza, pamoja na kushirikiana na hata
kuonekana kuhuzunika.
Kwa karne nyingi nyangumi
wamekuwa wakiwindwa kwa ajili ya nyama na malighafi. Kati ya karne
ya 20,
hata hivyo, viwanda vingi vya nyangumi
vilisababisha kuwa hatarini kwa spishi nyingi za nyangumi, na uwindaji
wa nyangumi ukakomeshwa
mara moja katika nchi nyingi isipokuwa chache.
Mashirika kadhaa
yameanzishwa kwa ajili ya kuzuia uwindaji wa nyangumi na hatari nyingine kwa
maisha ya nyangumi.
Cetacea wote, kujumuisha
na nyangumi na pomboo, ni kizazi kilichotokana na
mamalia wa nchi kavu wa oda ya Artiodactyl. Kwa pamoja cetacea na
artiodactyls sasa wanaainishwa chini ya oda moja ya Cetartiodactyla
inayojumuisha viboko na nyangumi.
Kimsingi, nyangumi wana ukaribu mkubwa na viboko; wote ni chimbuko la uzao mmoja, Indohyus, miaka takriban milioni 48 iliyopita na
wanyama wenye kwato shufwa kutoka Kashmir, India, karibu miaka milioni 54
iliyopita.
Nyangumi waliingia majini
karibia miaka milioni 50 iliyopita.
Cetacea wamegawanywa
kwenye makundi mawili:
·
Nyangumi-chujio (Mysticeti) wanaotambuliwa kwa aina
ya chujio katika domo lao
iliyoundwa kwa keratini na ambayo hutumika
kwa kuchujia planktoni kutoka majini. Hawa
ndio nyangumi wakubwa kuliko wote.
·
Nyangumi-meno (Odontoceti) wanaotumia meno yao kwa
kuwinda samaki na ngisi, na pengine (nyangumi mwuaji) mamalia wengine wa maji
kama sili na simba-bahari na hata nyangumi
wengine.
"Perkenalkan kita Sahabat303 Agen Sabung Ayam, Agen Bola Terpercaya, Casino Online, Slot Games.
ReplyDeleteDengan pendaftaran gratis dan mudah tentunya.
Hanya dengan Minimal Deposit 50 ribu anda sudah bisa bermain dan menikmati Berbagai Bonus Menarik Dari Sahabat303 Berikut Ini :
» Bonus Deposit 10% Khusus Sportbook
» Bonus Deposit 10% Khusus Bola Tangkas
» Bonus Rollingan Live Casino 0,7%
» Bonus Cashback Casino Games 2%
» Bonus Cashback Sabung Ayam 5 - 10%
» Bonus Cashback Sportbook 6 - 16%
» Bonus Refferal 2%
Moto kita »
Kemenangan berapa pun pasti kita bayar lunas.
Untuk Info Lebih Lanjut Silahkan Hubungi Kami Melalui :
* LIVE CHAT TERSEDIA , LAYANAN 24 JAM NONSTOP
* Website : Sahabat303
* LINE : sahabat_303
* WA 1 : +855882348077
* WA 2 : +6287705585269
* Telegram : @sahabat303
* FB : Sahabat303
DAFTAR SITUS JUDI ONLINE TERPERCAYA
Agen Sabung Ayam
Agen Bola
Agen Bandarq
Agen Togel Online"