#AFYA
Fahamu kuwa bamia
linaweza kukutoa katika hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari kwa sababu ya
uwezo wake wa kusaidia kuyeyusha au kumeng’enya sukari.
Pia, huweka sawa mfumo wa
sukari mwilini. Bamia ni aina tunda mboga yenye utajiri wa makapimlo ambayo ni
muhimu sana katika mwili hasa katika usagaji wa chakula.
Mara nyingi tumekuwa
tukichukulia bamia kama mboga ya kimaskini pasipo kujua ni tunda mboga lenye
faida nyingi sana.
Moja wapo ya faida ambayo
ni muhimu ni kusaidia kumeng’enya sukari mwili au kuweka sawa mfumo wa sukari
mwilini na pia tatizo la kukosa choo ni tatizo la kawaida kwa wagonjwa wa
Kisukari.
Bamia ikiliwa mara kwa
mara inasaidia kurekebisha mfumo wa umeng’enya chakula na sukari mwilini.
Maji maji yanayotoka
katika bamia yana uwezo wa kuondoa lehemu katika mishipa ya damu kwenye mwili.
Lehemu
ni aina ya mafuta yanayopatikana kwenye mishipa damu, endapo mafuta haya
yakazidi huweza husababisha maradhi ya shinikizo la damu.
Mgonjwa
wa kisukari mwenye shida ya lehemu muhimu kula bamia mara kwa mara.
Tukiachana
na kisukari, bamia huongeza na uboresha kinga ya mwili hasa kwa watu ambao
kinga yao ya mwili imeshuka kama watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi
(VVU).
Wataalamu
lishe wanasema watu wengi wamekuwa wakila bamia kwa kuidharau ila huzuia
magonjwa ya moyo kwa kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri.
Watu
wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, bamia huwasaidia kupunguza uwezekano wa
kupata saratani ya tumbo na huongeza kiwango cha damu mwilini. Wengine
wanatumia bamia kama dawa ya kuongeza kinga ya mwili kwa kutafuna zikiwa mbichi
au kuzichemsha.
Angalizo
kwa wagonjwa wa kisukari, msiache dawa zenu na kuanza kutumia bamia kama dawa.
Tumia bamia mara kwa mara kama tunda mboga linalosaidia kumeng’esha sukari
mwilini na kuimarisha kinga ya mwili wako.
Kwa leo tutakomea hapa,, share,like na koment wengine nao wapate faida.
No comments:
Post a Comment