MAPENZI KWA MDOMO NIHATARI,JIEPUSHE. - waleo blog

Breaking

Sunday 26 January 2020

MAPENZI KWA MDOMO NIHATARI,JIEPUSHE.



#AFYA

ORAL SEX (Mapenzi kwa njia ya mdomo)
Oral sex siku hizi imekua ikifanywa sana na makundi ya rika zote kwa kigezo cha kuridhishana kimapenzi.. Lakini mara nyingi hua kimbilio la wengi hasa wale wanaoogopa mimba na hata wale ambao majogoo wao huchelewa kuwika.

TUJIULIZE!! JE NI SALAMA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO!?
Kwanza tujue maana ya oral sex.
Ni kitendo cha mwanamme na mwanamke kunyonya/kunyonyana sehemu za siri wakiwa faraghani.

Madhara ya Oral sex
HUMAN HERPERSVIRUS (HHV-1 &-2)
Human Herpesvirus-1 (HHV-1) ni virusi ambao hushambulia sehemu za siri na kusababisha ugonjwa uitwao genital herpes. Mara nyingi ugonjwa huu hutokea baada ya Kufanya ngono kwa njia ya mdomo au kwa kitaalamu “oral-genital sexual intercourse”.
Human Herpesvirus-2 (HHV-2) pia husababisha malengelenge katika sehemu za siri..
Dalili hutokea baada ya siku tano baada ya kuambukizwa na virusi hawa. Sio mara zote watu wenye virusi hawa hutokwa na malengelenge sehemu za siri bali watu wengine wanaweza wasiwe na dalili yoyote ya virusi hawa na huambukiza wengine kwa urahisi zaidi kuliko yule mwenye malengelenge.
Mgonjwa anaweza kuhisi maumivu, kuungua, kuwasha, au unyeti wa ngozi kwenye maeneo ambapo Genital herpes wamezaliana. Maambukizi hutokea wakati herpesvirus inapovamia midomo, ulimi, au ngozi yenye vidonda au michubuko. Virusi zinaweza kubaki bila kusababisha ugonjwa kwa miaka mingi kabla ya kusafiri chini seli zna kusababisha dalili za mara kwa mara katika midomo, ulimi,sehemu za siri, vidole, au macho. Pia virusi vinaweza kusafiri hadi kwenye ubongo na kusababisha Kansa ya ubongo.

KANSA YA KOO
Oral sex au mapenzi kwa njia ya mdomo yanaweza kukusababishia kupata virusi vinavyoitwa Himan Papilloma (HPV) ambavyo hushambulia koo na baadae unaweza kupata kansa ya koo.
Syphilis lesions (malengelenge ya kaswende)
Malengelenge ya kaswende hua yanatokea katika sehemu za siri na mara chache kwenye chuchu za maziwa. Lakini malengelenge hayo yanaweza kutokea kwenye midomo kama utafanya mapenzi ya mdomo na mtu mwenye ugonjwa huo.

Chlamydia trachomatis
Bacteria hawa wamekua wakiwashambulia sana vijana katika miaka hii ya karibuni. Mara nyingi vijana wengi hukutwa na bakteria hawa ndani ya koo zao. Na inaaminika wameambukizwa kwa kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo.
Lakini kumbuka kua kama bacteria hawa watazaliana katika koo, mdomo au pia, wanaweza kusababisha maambukizi katika macho na kukusababishia ugonjwa wa macho ambao hautibiki kwa dawa zile za maji za kutibu macho na baadae unaweza kupata upofu.
HEPATITIS  A
Hawa ni virusi ambao husababisha maumivu ya tumbo na jaundice au ugonjwa ambao husababisha ngozi kua ya njano. Jaundice ni ugonjwa hatari sana ambao tunaweza kumsababishia mgonjwa kufa baada ya mda mfupi.
Hepatitis A virusi hupatikani kwa wingi kwenye kinyesi au sehemu za haja kubwa. Mapenzi kinyume na maumbile husababisha kupata virusi hawa.

HEPATITIS  B
Virusi hivi hulingana sana na Hepatitis A, lakini Hepatitis B husababisha ugonjwa mkali na hatari wa ini na huaribu ini.
Mara nyingi huambukizwa kwa kuchangia damu ambayo ina virusi hivi kwa njia ya sindano, vitu vyenye ncha Kali au kuwekewa damu hospitalini yenyewe virusi hivi.
Lakini chembe chembe za virusi hivi hupatikana pia kwenye shahawa au semen, kinyesi au sehemu za haja kubwa, mate na pia damu. Imethibitishwa kua Mapenzi kinyume na maumbile huleta maambukizi haya.

Bowel bakteria.
Salmonella, Shigella and Campylobacter ni bakteria ambao wanaweza kusafirishwa kwa njia ya mdomo-na njia ya haja kubwa. Salmonella na Shigella husababisha ugonjwa mkali sana wa kuharisha.
Haya ni baadhi ya madhara ambayo unaweza kuyapata.

Usisahau ku-share,maoni,like,koment ili elimu hii iwafikie watu wengine..

No comments:

Post a Comment

Pages