#TIBA
MBADALA
TAFADHALI NDANI YA MAKALA
HII KUNA MISAMIATI AMBAYO INAWEZA KUKUKERA,UTUSAMEHE.LENGO NI KUPEANA ELIMU KWA
UFAHAMU WA WATU NA WENGINE NAO TUELIMIKE.
1.AASHIKI (PENDA PENDA)
Hii ni aina ya jini mahaba ambayo ndani yake wapo wakike na wakiume kama tulivyoona katika makala iliyopita ya historia ya majini.Jini huyu humwingia mwanaume ama mwanamke aliyempenda kwa jinsia zao.Jini huyu huyu pia miongoni mwao wapo pia wanaotamani kuwaingilia watu kinyume na maumbile (kuwalawiti) wengi wetu tumezoea kumwita popobawa.
1.AASHIKI (PENDA PENDA)
Hii ni aina ya jini mahaba ambayo ndani yake wapo wakike na wakiume kama tulivyoona katika makala iliyopita ya historia ya majini.Jini huyu humwingia mwanaume ama mwanamke aliyempenda kwa jinsia zao.Jini huyu huyu pia miongoni mwao wapo pia wanaotamani kuwaingilia watu kinyume na maumbile (kuwalawiti) wengi wetu tumezoea kumwita popobawa.
Kuna dalili nyingi za kumjuza mwanaume wa kibinadamu kuwa anasumbuliwa na jini mwanamke. Baadhi ya dalili hizo ni kama ifuatavyo:
1. Ndoto nyingi mbaya na za hovyo-hovyo,
2. Mtu huona kama vile kitandani kwake kuna mtu lakini haoni kitu
3. Mtu huona kuwa tamaa yake ya ngono huongezeka mno pale mkewe anapokuwa hayupo, lakini mkewe akiwepo hukosa hamu naye.
4. Kabla ya kuoa, mtu alikuwa na hamu kubwa ya mke lakini baada ya kuoa hukosa hamu ya mke.
5. Mtu huota yuko pamoja na watu wa jamii fulani na anapoamka hujihisi kuchoka
6. Mtu husikia harufu ya manukato bila kujua inatokea wapi
7. Mtu huweza kusikia mtu anatweta au kushusha pumzi sikioni mwake kitandani lakini haoni mtu.
8. Mtu hupoteza hamu ya mwanamke na hatamani tena kuoa mke, na hutoa visingizio vingi vya kukataa kuoa
9. Mtu kupenda kufuatilia, kutazama-tazama na kushika-shika sana sehemu zake za siri na kujiwa na hamu ya ngono.
10. Kila anapokuwa karibu na mkewe ndivyo hamu ya kuingiliana naye inavyotoweka lakini mke anapokuwa mbali ndipo hamu humjia
11. Mtu huwa na hamu kubwa ya wanawake wengine badala ya mkewe.
12. Mtu kuwa na hamu kubwa ya ngono ya zinaa kuliko ngono halali ya kukutana na mkewe.
13. Mwanamke mwingine anapokaa na mkewe, mtu huwa na hamu zaidi na mwanamke huyo mwingine kuliko mkewe. Kama vile kutamani shoga wa mkewe
14. Mtu hujisikia vibaya na kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na mkewe
15. Mume hutokea kumchukia tu mkewe bila sababu. kila siku visirani haviishi
16. Mtu kushikwa na usingizi mzito muda wa kukutana na mkewe kiunyumba, hata mkewe akimuamsha, haamki na hukasirika kuamshwa
17. Ndoto za kufanya zinaa na wanawake mbalimbali ambao mtu anawajua.
18. Mtu kukuta unywele mrefu katika nguo yake ya ndani, unywele huo haufanani na nywele zake
19. Kama mtu analala chumba kimoja na watoto wake wadogo, watoto huamka ghafla na kutaka kukimbia. Au mtoto huamka na kuelekea mlangoni kufungua mlango huku akilia. Mtoto hulalamika kusikia maumivu sehemu za siri. Hapo kuna mwanamke Jini ambaye anataka watoto hao waondoke ili apate nafasi ya kuwa na wewe.
DALILI
ZA MWANAMKE MWENYE JINI MAHABA
*Huota anaingiliwa kwenye ndoto,
*Huota anazaa akiwa kwenye ndoto,
*Huota ananyonyesha,
*Huota anaolewa au kuveshwa pete,
*Hukosa hamu ya tendo la ndoa,
*Huchukia wanaume,
*Huachika katika mahusiano mara kwa mara,
*Mimba kupotea mara kwa mara au kutoka.
TOFAUTI YA NDOTO ZA KAWAIDA NA NDOTO ZA KIJINI
Ndoto za kawaida
1. Ndoto inayotokea baada ya balekhe ambapo mtu hutokwa na maji ya uzazi, hii ni ndoto ya kawaida.
2. Hakuna uchovu mtu anapoamka licha ya kuota anafanya kitendo cha ngono, hii ni ndoto ya kawaida.
3. Ndoto za kuota kitendo cha ngono zinazokuja kwa nadra labda tuseme mara tatu kwa mwezi. Hii ni ndoto ya kawaida.
4. Ndoto hudumu sekunde chake.
Ndoto za Kijini
1. Mtu huota-ota ngono kila siku. Huyu ni Jini anayesumbua
2. Mtu huota na huhisi viungo vyake vya siri vinagusana na vya mwanamke asiyekuwepo. Huyu ni Jini anayesumbua
3. Ndoto ya kufanya ngono huchukua muda mrefu kutegemeana na nguvu za mtu hadi anapotokwa na maji ya uzazi, au anapoamka ghafla huku dhakari ikiwa imenyooka na moyo kumwenda mbio.
4. Kama mtu ataamka akiwa amechoka sana baada ya ndoto ya kufanya kitendo cha ngono.
5. Mtu akijihisi ndotoni kuwa analifaidi mno tendo la ngono.
6. Ndoto ya kitendo cha ngono inayotokea mara kwa mara, mathalani, tuseme mara tatu kila wiki, au wakati mwingine, kila siku, na wakati mwingine kila anapolala au kupata usingizi hutokewa na ndoto hiyo ya kufanya kitendo cha ngono, na wakati mwingine, hata mara tatu kwa siku.
Maingiliano ya kingono baina ya wanadamu na majini yanajumuisha mambo manne
1. Al-Ihtilaam
Kila kitu, kuanzia starehe hadi kutokwa na manii hutokea akiwa ndotoni, na inamlazimu mtu kufanya josho
2. Al-Istimtaa
Mtu hufaidi kitendo cha kumuingilia mwanamke wa Kijini lakini bila kumwaga maji ya uzazi. Anapoamka mtu huyu halazimiki kufanya josho (kuoga).
3. Al-Mu’asarat
Kitendo cha Jini kuingiliana na mwanadamu. Mwanadamu hujua kuwa anamuingilia Jini lakini bado hushindwa kuacha kitendo hicho.
4.Al-Taksiil
Ndoto humtokezesha Jini kwa kiwiliwili chake ili aingiliane na mwanaume wa kibinadamu. Hii ni hatua ya mbali na ya hatari sana. Wakati mwingine, watu hudhani kuwa wanapata matatizo au “mikosi” kwa sababu ya wake waliowaoa lakini kumbe ni Mwanamke Jini anayeleta fujo kwa sababu ya ‘mwanaume wake’ kuoa mke. Mwanamke jini hufanya hila na vituko vya kutishia au kuhatarisha maisha yako ili umwache mkeo wa kibinadamu.
Njia za kumwezesha Mtu kujikinga na Kitendo cha Kuingiliana na mwanamke jini
1. Paka miski nyeusi au nyekundu sehemu za siri. Na kama hakuna miski, basi paka maji ya waridi au mafuta ya mzeituni.
2. Paka mafuta ya mzeituni mwili mzima, na habati sawda, pamoja na ruqya ya kusoma aya za Qur’an kila siku, na kabla ya kulala.
3. Nyunyizia au tonea manukato ya miski nguo za kulalia.
4. Usilale bila nguo au usilale na nguo za kuonesha maungo ya ndani. Lala ukiwa umevaa
5. Kusema Bismillah wakati wa kuvaa, hii ni kwa mujibu wa Hadith ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake.
6. Kuleta nyiradi nyakati za asubuhi na jioni hasa nyiradi za kabla ya kulala.
7. Jiepushe na dhambi na timiza faradhi zote.
8. Usilale-lale kama inawezekana.
9. Dua kwa Mwenyezi Mungu akukinge na Shetani.
Kwa ufumbuzi, ushauri kwa wenye dalili mwiongoni
mwa hizo,, tafadhali mtafute mtaalamu wa tiba hizi..
Jumasaidy2328@gmail.com/0712172328
No comments:
Post a Comment