#SHAIRI
Hii ndio tamaduni,zetu
halikujuzana,
Nitumaini jemaa, kwangu nyote niwazima
Mashindano
ya silaha,.hatari kwa binadamu.
2.Si mpira uwanjani, ama rumba ukumbini,
Si resi
barabarani ,ama kwaya kanisani,
Ni silaha shindaneni, iletayo upinzani,
Mashindano ya silaha ,hatari kwa binadamu.
3.Hawalali
mitamboni, kila siku wanabuni,
Wabuni ‘’tufanyenini, kumshinda Marekani,
Kipanki
asifaulu,ajetupiga mwakani,’’
Mashindano ya
silaha,hatari kwa binadamu.
4.Silaha za aridhini,zinginezo za angani,
Zinategwa baharini,pia zingine hewani,
Zaundwa ziuwe nani,kama si mjamanani,
Mashindano ya silaha,hatari kwa binadamu.
5.Gharama matilioni, mengi yasiyo kifani,
Yaishia mitamboni, kulekule viwandani,
Kuunda
wanazo buni,silaha kali motoni,
Mashindano ya
silaha,hatari kwa binadamu
.
6.Zipo nchi masikini, pande zote duniani,
Msaada
wanatamani ,kuinua maishani,
Hawapewi
asilani, hatawalie machoni,
Mashindano ya silaha,hatari kwa binadamu.
7.Uchochezi namba wani,kuchokoza nchi duni,
Zingine
mapiganoni,wao wakae pembeni,
Silaha
kwenye medani,zitumwe majaribuni,
Mashindano ya silaha, hatari kwa binadamu.
8.Tuundieni mashini, zakulimia shambani,
Maji
tuna yatamani,yatukidhi vijijini,
Chakula
pia leteni,mafuta ya paretoni,
Mashindano ya silaha, hatari kwa binadamu.
9.Shairi
hi tamatini, kwenu ninawaombeni,
Silaha
hizo acheni,kuziunda viwandani,
Manayake
hatuoni, yasilaha duniani,
Mashindano ya silaha, hatarikwabinadamu.
,
No comments:
Post a Comment