Kwa mujibu wa Shirika la Afya la duniani
(WHO) ili kuwa na afya njema na kujenga mwili imara,unahitajika kufanya mazoezi mepesi angalau kwa dakika 150 kwa wiki yaani kwa siku dakika 30 katika siku
tano za wiki.
Muda huo ndiyo unatupa faida za kiafya
zifuatazo ambazo unaweza kuzipata endapo utayafanya mazoezi haya kwa ratiba.
1.Kukukinga na magonjwa
Kupunguza hatari ya kupata magonjwa
yasiyoambukiza ikiwamo magonjwa ya moyo, kiharusi, saratani na kisukari kwa
sababu mazoezi yanasaidia kuwa na mfumo wa moyo na damu yenye afya njema.
Unene ni kihatarishi cha kupata magonjwa
mbalimbali yasiyoambukiza, kufanya mazoezi kunashughulisha viungo vya mwili
hivyo kuchoma mafuta yaliyorundikana hatimaye kudhibiti uzito uliokithiri.
3. Kushusha shinikizo
Mazoezi yanasababisha kuwa na moyo na
mishipa ya damu yenye afya njema kuchangia kushusha shinikizo la juu la damu
ambalo ni sawa na tendo la uuaji wa kimyakimya.
4. Mfumo wa hewa
Kufanya mazoezi kama kutembea, kukimbia
na kuogelea kunasaidia misuli ya mwili kuwa na ufanisi wa juu kusafirisha na
kutumia oksijeni katika mapafu pamoja na kutoa hewa chafu nje ya mwili.
5. Mfumo wa chakula
Mazoezi yanakufanya kuwa na hamu ya
chakula na maji, husaidia chakula kusagwa, kunyonywa na kutolewa kwa ufanisi
mwilini na kukuepusha na tatizo gesi na ukosefu wa haja kubwa.
6. Kupunguza hatari ya kupata saratani
Tafiti zinaonyesha wanaofanya mazoezi
huondokana na hatari ya kupata saratani za ziwa, utumbo mpana na mapafu
ukiwalinganisha na wasiofanya.
7. Kudhibiti lehemu mbaya
Lehemu (cholesterol) ni mafuta ndani ya
mishipa ya damu, mazoezi yanapunguza kiwango cha lehemu mbaya na kuongeza
kiwango cha lehemu nzuri ambayo ina faida mwilini.
Lehemu mbaya ndiyo inaharibu mishipa ya
damu ikiwamo ya moyo, hivyo kuidhibiti hupunguza hatari ya shambulizi la moyo
(heart attack) na kiharusi (stroke).
8. Kinga imara
Kadiri unavyofanya mazoezi mara kwa mara
ndivyo hatari ya kuumwa na magonjwa mbalimbali inavyopungua hii ni kutokana na
mazoezi kukufanya kuwa na kinga madhubuti dhidi ya vimelea.
Kuimarisha misuli na kukupa ukakamavu wa
mwili kwasababu mazoezi yanaifanya misuli kujengeka na kudumu, hivyo kuweza
kukabiliana na mazingira magumu.
10. Maungio
mepesi
Kusaidia maungio na viungo vya mwili
kuwa myepesi hivyo kufanya matendo mbalimbali ya kimwili kwa haraka na ufanisi
pasipo kupata majeraha kirahisi.
11. Mifupa imara
Kusaidia kuwa na mifupa imara
iliyojengeneka, hivyo kupunguza hatari ya kupata tatizo la kumomonyoka mifupa
lijulikanalo kitabibu kama Osteoporosis.
13. Usingizi mnono
Kuchangia kupata utulivu kimwili, hivyo
kupata usingizi mnono. Usingizi una faida kwa mwili ikiwamo kusahihisha
hitilafu mbalimbali za mwilini na kujenga kinga imara na mwili
14. Kuboresha afya ya akili
Kemikali ijulikanayo kama Endophins inayozalishwa
wakati wa ufanyaji wa mazoezi husababisha mwili kupata hisia nzuri ikiwamo
furaha.
Vilevile mazoezi humsaidia mtu
kupeperusha hisia hasi ikiwamo hofu, woga, sonona (depression) na kumfanya
ajihisi ni mtu mpya.
15.Mienendo
Kujenga utegemezi na mazoezi na kuyazoea
sana husaidia kushikamana nayo, hivyo kukuepusha na vishawishi ikiwamo mienendo
na mitindo mibaya kama vile utumiaji tumbaku, ulaji holela wa vyakula, ulevi na
uasherati.
16. Kuondoa sumu
Wakati wa mazoezi jasho hutoka kwa wingi
pamoja taka sumu na maji ambayo hutoka pamoja na joto lililozidi, hivyo
kusaidia kulinda joto la ndani ya mwili.
17. Kuboresha ngozi
Kutoa taka sumu yaani jasho kunaisafisha
ngozi na kuifanya kuwa na afya, vilevile misuli iliyotuna huifanya ngozi
kuvutika na kuwa ng’avu ndiyo maana wanaofanya mazoezi huonekana wenye afya na
wasiozeeka.
18. Hamu ya kunywa maji mengi
Kupata kiu baada ya kutokwa jasho
hukufanya kunywa maji kwa wingi. Maji yana faida lukuki kiafya ndiyo maana
unaweza kuishi bila chakula lakini si bila maji.
Maji hurudishia maji na chumvichumvi
zilizopotea kwa njia ya jasho wakati wa mazoezi, hivyo kukufanya kuendelea kuwa
na mzunguko mzuri wa damu.
19. Kuondoa uchovu na maumivu
Uchovu husababisha hisia za mwili kuuma,
mazoezi huondoa mrundikano wa tindikali ya Lactic ambayo ndiyo inasababisha
uchovu, maumivu na kukakamaa au kuwaka moto kwa misuli. Vilevile kupunguza
maumivu wakati wa hedhi kwa wanawake.
20. Tendo la ndoa
Mazoezi huongeza uimara wa misuli
ikiwamo ile ya misuli ya kitako cha kiuno ambayo ndiyo inayoongeza ufanisi
katika tendo la ndoa kwa pande zote mbili, hivyo kuimarisha uhusiano.
21. Nguvu za kiume
Mazoezi husaidia kuongeza nguvu za kiume
kwa kuchochea kuzalishwa kichochezi cha kiume, kudhibiti unene uliokithiri,
utiririkaji wa damu katika misuli ya uume na kuondoa woga wakati wa tendo.
Mazoezi humsaidia mwanamke mjamzito
kuiandaa misuli ya kiuno na nyonga kutanuka vyema ili kuwezesha kujifungua
salama. Pia, kumfanya kuwa na ustahimilivu na nguvu za kumsukuma mtoto
anapozaliwa.
No comments:
Post a Comment