KANUNI 10 BORA, ZA KILIMO ( HAKUNA UCHAWI ) - waleo blog

Breaking

Saturday 21 December 2019

KANUNI 10 BORA, ZA KILIMO ( HAKUNA UCHAWI )


#KILIMO BORA


 Watu wengi tumekuwa tukilalamika ya kuwa, mbona tunalima mashamba makubwa! Lakini mazao machache?. Leo nikupe kanuni kumi ambazo zinakubalika na kuaminika katika kuwakomboa wakulima kiuchumi na kwa mahitaji yao ya chakula iwapo zitazingatiwa. Kanuni hizo ni:

Kitaalamu, shamba lifaalo linapasa kuwa eneo lenye ardhi yenye rutuba, historia ya kutokuwa na magonjwa mengi ya mimea na wadudu waharibifu, kuwapo kwa miundombinu kama barabara, mawasiliano, maji na hali nzuri ya hewa na lisiwe mbali na soko la mazao yatokayo shamba.

 Husaidia uboreshaji wa mazao katika msimu unaofuata, mkulima anaweza kuyatumia masalia ya mazao ya msimu uliopita shambani kwa
kuyachanganya na udongo na kuwa chanzo cha mbolea hai ambayo hurutubisha udongo shambani. Vilevile kwa kulainisha udongo wakati zoezi hili likifanyika husaidia kurahisisha hewa kupenya katika udongo ambayo ni muhimu kwa wadudu mbalimbali waishio ardhini kurutubisha udongo, Kadhalika hurahisisha mizizi ya zao husika kupenya kirahisi kutafuta virutubisho na mbegu kuota kirahisi.

3. KUCHAGUA MBEGU BORA:

 Mbegu bora ni zile zilizoboreshwa ili ziweze kutupatia mavuno zaidi, zenye kustahimili ukame, magonjwa na wadudu. Kwa kutumia mbegu zenye ubora wa namna hiyo kutatupa ufanisi na uhakika wa kupata mavuno mengi zaidi.

4. KUPANDA MAPEMA NA KWA NAFASI:
Husaidia mimea iliyomo shambani kutumia vyema virutubisho mbalimbali vilivyomo kwenye udongo na pia kusaidia mmea kusharabu mwanga wa jua na hivyo kuweza kujitengenezea chakula ambacho ni muhimu kwa makuzi yake na hivyo kutupatia mavuno ya kutosha.

5. KUPALILIA MAPEMA:
Kupalilia kuna faida nyingi kwa mazao yetu kama vile kulainisha udongo na kurahisisha mbegu kumea vizuri, mizizi iweze kupenya kirahisi wakati ikisaka virutubisho kwenye udongo, kuruhusu hewa kupita kirahisi ambayo ni muhimu kwa uhai vijidudu mbalimbali vinavyoishi ardhini ambavyo hurutubisha udongo.

6. KUPUNGUZA MICHE:
 Hii husaidia mimea inayobakizwa shambani kuweza kutumia virutubisho vilivyomo ardhini kwa kiasi cha kutosha hivyo kumea vyema na
kuweza kutoa mavuno mengi.

7. KUTUMIA MBOLEA ZA KUPANDIA,KUKUZIA NA KUZALISHIA:
 Mbolea ina faida ya kusaidia mimea kumea na kukua vyema vilevile huikinga mmea dhidi ya mashambulizi mbalimbali ya magonjwa wadudu hivyo kuweza kukua vyema na kutoa mazao mengi yenye ubora wa kutosha.

8. KUZUIA WADUDU NA MAGONJWA:
 Husaidia mimea kusitawi vyema na kwa haraka na huo ndiyo msingi wa kupata mavuno mengi. Iwapo magonjwa na wadudu hawatadhibitiwa kwa wakati muafaka kuna uwezekano mkulima kushindwa kabisa kupata mavuno au kupata mavuno machache.

9. KUVUNA KWA WAKATI NA KUHIFADHI:
Inashauriwa Kuvuna mazao yetu wakati yakiwa yamekomaa vilivyo kwani kuvuna mapema licha ya kuharibu ubora wa zao husika pia inakuwa ni vigumu kuyahifadhi kwa usalama na hata kama yakipelekwa sokoni kuna uwezekano mkubwa mkulima akashindwa kuuza zao lake kwa bei inayostahili. Kwa mfano mkulima anapovuna mahindi kabla ya kukomaa na kukauka inakuwa vigumu kuyahifadhi ghalani na atapoyafikisha sokoni itabidi kuyauza kwa bei yeyote haraka ili kuepuka yasiharibike.

10. KUBADILISHA NA KUTUMIA KILIMO MSETO:

Ina faida ya kuwezesha zao moja kutumia rasilimali ya zao lingine kuweza kukua vyema na kutoa mavuno mengi. Mfumo huu pia humsaidia mkulima kupunguza hasara mbalimbali za shambani kwa mfano iwapo zao moja halikutoa mavuno ya kutosha basi kuna uwezekano wa zao lingine kufanya vizuri na hivyo kupunguza athari kubwa ambayo mkulima angeweza kupata kama angeamua kupanda zao moja. Vilevile husaidia kupunguza mazaliano ya wadudu na magonjwa ambayo yamezoeleka kwa aina moja ya zao

No comments:

Post a Comment

Pages