#UTALII
Simba ni
mnyama wa pili kwa ukubwa katika wanyama jamii ya paka duniani, sio hivyo tu
nani wa 1 [kwanza] kwa ukubwa barani Afrika.Wa kwanza ni Puma [Tiger] na wanyama wengine jamii ya paka yaani Chui, Duma, paka wa dhahabu na paka wa nyumbani.Simba wanapatikana katika mbuga zote nchini.Simba
wanapenda kuwinda wanyama wakubwa kwa ajili ya chakula, kama vile Nyumbu,Nyati,
Punda milia na wengine wakubwa.’’Loooooooh!!!!! niweke angalizo hata mimi mwandishi na wewe msomaji wa makala
hii tukijichanganya kwa Simba huenda tukawa msosi kwao.Hivyo basi tuwe makini tuingiapo
hifadhini kufanya utalii .Lakini pia tuepuke uindaji haramu yaani ujangili,maana ni hatari ukikutana na mnyama kama jamii ya
Simba’’.Simba dume ni mkubwa kuliko
Simba jike.Tofauti kati ya dume na jike
ni; Simba dume ana kichwa kikubwa na ni
mwenye nywele nyingi na ndefu shingoni mwake ziitwazo [mane].Pia Simba dume lina uzito wa kilo 200-250. Simba jike yeye
hana kichwa kikubwa wala nywele nyingi na ndefu shingoni mwake.Simba jike yeye
ana uzito wa kilo 120—150. ‘’Dah wacha nishangae kidogo na kutafakari maisha ya
myama huyu, yaani jike huhimili uzito wa kilo 50—100 za mmewe? Kweli simba jike
pia ni mvumilivu wa ndoa yake.Wake zetu sasa ungesikia__________..haya
bwana ‘’. Pia simba jike
ndio mtafutaji chakula{ mwindaji} na dume ndie huwa mlinzi wa
familia.’’kikwetu kwetu hapa utasikia,, baba Yule mvivu kweli mara
anamtesa mkewe mhh! wakati haki sawa kwa wote’’.
Simba huwa
hawali chakula kila siku,yaani simba akiwinda mnyama leo na wakala wakashiba, basi hukaa na shibe hiyo
ndani ya siku tano[5] mpaka saba[7] ndio wale tena.
Fungate(honeymoon) makubwa kweliii!!! Kumbe simba ndivyo walivyo
’’ha ha haaaaaa
Simba wakisha jamiiana na kupata ujauzito basi hulea
ujauzito huo ndani ya miezi mitatu [3] na huzaa watoto 4-5. Hapa simba huwa ni mkali sana kwa
kuwa huhitaji kuwatunza wanawe wakue kwa
salama na amani.
Simba
huishi miaka 20-25 na baada ya hapo ni umauti, kama ilivyo ada kwa viumbe
wote..
Adui mkubwa
wa simba ni binadamu na maradhi.
Huyu ni Simba kwa uchache sana hali na tabia zake.
Usisahau kutufuata
(follow)na kutoa maoni ama ushauri
wowote ule katika makala na habari mbali mbali.
Kwa mambo yote
kuhusiana na utalii usisite kututembelea katika:-
malamboaziz14@gmail.com/0717475992/0782080716
Use english please
ReplyDelete