📚 TABIA YA KUGHAIRISHA SEHEMU 2⃣
MUENDELEZO.
➡ SABABU YA KISAIKOLOJIA KUHUSU KUGHAIRISHA MAMBO.
Katika sehemu iliyopita tuliangalia sababu ya kisayansi
kuhusiana na tabia hiyo.
➡ utafiti wa
kisaikolojia ulibaini watu wengi hupenda kuwaza,kuangalia na kufanya vitu kwa
sura ya nje kwasababu ya MAZOEA.
Watu wanaishi maisha yao kwa MAZOEA. Katika kitabu cha
sayansi ya tabia kinasema tabia zote nzuri na mbaya ni matokeo ya mazoea ya
kurudiarudia mambo.
Utafiti wa
kisaikolojia unaonesha ili uweze kuidhibiti tabia ya kughairisha mambo
unatakiwa utambue umeathirika na mazoea yapi yanayopelekea tabia hiyo.
➡Kuna aina au makundi saba (7) ya watu katika tabia ya
kughairisha mambo.Hiyo imefafanuliwa katika kitabu kijulikanacho kwa jina la
VIZUIZI VYA KUGHAIRISHA ( Ant procrastination).
🌐 Tuangalie aina moja hadi nyingine.
1⃣ Kundi la watu
wanaopenda kufanya vitu bila kujali chochote.
Watu hawa hufanya chochote atakachokiona au kusikia mbele
yake kwasababu tu anaamini atapata kitu au kumlipa.Kwa kifupi hili ni kundi la
watu wasio na vipaumbele katika maisha yao. Hufanya vitu kwa msukumo tu wa
matokeo na sio kufanya vitu kwa kumaanisha,kwasababu hiyo ni rahisi sana
kupoteza uvumilivu wanapo kosa au kuchelewa kupata matokeo na kupelekea
kughairisha.
2⃣ Kundi au aina ya watu wanaoghairisha kwasababu ya kutojua
hatua za kuzifuata katika kazi au jambo husika.Watu hawa hupenda na fufanya
vitu lakini hufanya bila kujua na kufuata njia sahihi katika kazi hiyo na
kumpelekea kutofikia kiwango kikubwa cha matokeo,hiyo huwaumiza na kupelekea
kukata tamaa na hatimaye kughairisha
3⃣ Kundi au aina ya watu wanaoghairi kwasababu ya kusubiri
mpaka mambo yote yakae vizuri.Utasikia nikipata fedha kiasi fulani au nikijaliwa nitafanya
biashara furani.
4⃣ Kundi au aina ya watu wanaojiona wanamambo mengi kiasi cha
kukosa nafasi ya kufanya mambo au kazi nyingine.
Mara nyingi hawa ni wale watu wanaoona au kuzani kila kazi
lazima wafanye wenyewe hawafikirii kukabidhi majukumu kwa watu wengine.
5⃣ Watu wanaoona hawana muda wa kufanya mambo kwa sasa na
wanaamini watafanya wakipata muda.
6⃣ kundi au aina ya watu wanaoghairisha kwasababu ya kusahau
mambo au vitu.
Kusahau kunaweza sababishwa na mambo mengi,kupuuza,kutoona
umuhimu,kuhisi kushindwa n.k
7⃣ Kundi au aina ya watu wanaofanya mambo kwa kuangalia watu
wengine.
Watu hawa wamegawanyika katika makundi mawili
(I) Wale wanaoepuka lawama.Wanahisi watu wanafuatilia mambo
yao hivyo watamuonaje atakapo fanya hiyo kazi.
(II)e Wale wanaopenda wakifanya jambo wasifiwe.
Watu hawa wasiposifiwa huhisi kama kazi au jambo hilo
halifai.
✳ Hayo ndio makundi au aina saba za watu katika tabia ya
kughairisha mambo.
Katika sehemu ya pili ya somo hili tutaangalia kundi moja
baada ya jingine kwa undani na namna ya kujinasua katika hiyo hari
inayokuathiri.
✳ Je wewe una angukia katika kundi lipi kati ya hayo saba
tuambie. Itaendelea.............
By
Sixbeth Msita kutoka 🇹🇿 MSITA SUCCESS CLINIC🇹🇿
0692786550
No comments:
Post a Comment