RAIS MAGUFULI AWAONYA WAFANYA BIASHARA - waleo blog

Breaking

Monday 3 June 2019

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAFANYA BIASHARA




Rais Magufuli amempongeza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wote ambao wamesimamia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa tangu mwaka 2016 kuhusu kuondoa matumizi ya mifuko ya plastiki kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, Rais Magufuli amewataka wafanyabiashara kutotumia mwanya huo kuuza mifuko na vifungashio  mbadala kwa bei kubwa na badala yake amewataka wafanyabiashara hao pamoja na wawekezaji wa ndani na nje kujenga viwanda vya kutengeneza mifuko na vifungashio kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini.

Aidha, Rais Magufuli ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuwa na vifaa vya kubebea bidhaa wanazozinunua madukani na masokoni ili kuepuka gharama kununua vifungashio ama mifuko mbadala.

 
RAIS MAGUFULI “USILAZIMISHWE KUNUNUA MFUKO BEBA HATA KWENYE GAZETI, NDOO AU KITAMBAA”

 

No comments:

Post a Comment

Pages