BALLON D'OR
Ronaldo kwa sasa ana mfadhaiko mkubwa baada ya klabu yake
mpya,Juventus kutimuliwa ligi ya mabingwa na Ajax katika hatua ya robo fainali.
Labda turudi nyuma hadi 2006,ambapo mshindi wa Tuzo ya
Ballon d'Or hakufika hata hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa lakini hata
hivyo,Fabio Cannavaro alibeba Kombe la Dunia mwaka huo.jambo hili liliondoa
kelele za ushindi huo.Ikumbukwe kuwa mwaka huo Ronaldinho alishinda taji la
'Conferedation CUp' na timu yake ya taifa,Brazil huku taji lingine alilokuwa
akilitumaini ni La Liga pekee.
Licha ya kuwa alikuwa na magoli 13,usaidizi(assists) 16 na
ufundi mwingi uwanjani,hii haimkufanya ampiku mshindi wa mwaka huo,Cannavaro!
Labda hii inaweza kuwa sawa na mshindi wa Ballon d'Or kuwa
K. Mbappe huku taji analoshindania nalo Ligue 1 pekee.
Hata hivyo si mara zote mafanikio ya timu yakampa mchezaji
Ballon d'Or.Walikuwepo kina Sneijder na Frank Ribery miaka ya 2010 na
2013,licha ya mafanikio ya timu zao lakini hawakufua dafu.
Kwanini mtu ashinde tuzo hiyo?....Leo hii ni dhahiri kuwa
Ronaldo amejiweka mbali na ndoto ya kutwaa Ballon kwa mara ya sita.Wakati
mpinzani wake mkubwa (Messi) akijiweka siti ya mbele kuchukua tuzo hiyo.
"Hata kama hatachukua UEFA,lakini bado mesi anastahili
kushinda Ballon d'Or". Rivaldo,mwanzoni mwa wiki hii.
"....amekuwa akifunga,akitoa 'asisti',amekuwa mfungaji
bora wa La Liga kwa muda mrefu,na sasa anafanya hivyo ligi ya mabingwa,"
Ikumbukwe kuwa,baada ya Ronaldo kutolewa kwenye ligi
aipendayo,Messi alikuja juu akiifungia timu yake mabao mawili na kuipeleka nje
ya mashindano Manchester United na sasa anaisubiri Liverpool katika nusu
fainali.
"Messi ni mchezaji bora wa dunia,na ameonesha hivyo
kwenye mchezo wa leo".Jesse Lingard aliongea baada ya mechi.Maneno yake
yanatiwa na nguvu na kocha wake,Ole Gunnar ambaye alisema "Niseme tu Messi
ni mchezaji bora na leo alikuwa hivyo".
Messi na magoli 45 na usaidizi mara 21 katika michezo 42
msimu huu,rekodi hii inamfanya kuwa bora miongoni mwa wsenzake huko Ulaya.Huenda
Messi akimpiku Ronaldo kwa kutwaa Ballon d'Or ya sita,hii inakuja baada ya
ronaldo kuondolewa kwenye ligi aliyokuwa anaitegemea miaka ya hivi karibuni.
"Sijaona mchezaji bora kama Messi".Nahodha wa
zamani wa Barcelona,Josep Maria aliiambia redio MARCA.
...muda mwingi nilidhani Pele na Di Stefano walikuwa
bora,lakini Messi anakaa mbele yao,huyu Muajentina atashinda Ballon d'Or"!
Beki kisiki huko Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi,Van
Dijk,anaongoza safu ya ulinzi ya Liverpool,na mwaka huu ataongoza timu yake
taifa kwenye UEFA Nations Leaugue ikiwa ni katika cha mwaka mmoja tangu
waliposhindwa kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Urusi.
Raheem Sterling,anatajwa tajwa kutokana na mchango wake
katika klabu yake ya Manchester City ambayo ndiyo mpinzani mkubwa wa Liverpool
katika kutwaa taji la ligi kuu Uingereza msimu huu.Hata hivyo kuondelewa kwa
klabu yake kwenye ligi ya mabingwa kunamuweka mbali na tuzo hiyo.
Luis Suarez na Allison pia wanawekwa mstari wa mbele,wao ni
kama Messi,watakuwa kabiliana na Kombe la Mataifa bara la Amerika(Copa America)
mwaka huu.Na Mohamed Salah atakuwa na kibarua cha kuibeba Misri kwenye
AFCON,mashindano yatayofanyika nyumbani kwao.
Lakini miongoni mwa washambuliaji wanaodokezwa,Messi
anawazidi kwa mambo muhimu katika kunyakua Ballon d'Or,labda kwa Luis
Suarez,lakini na yeye ana kazi kubwa ya kumpita mwenza wake,Lionel Messi.
Ronaldo anaweka rekodi ya kushinda Premier league,La Liga na
Serie A.Lakini ndoto yake ya kutwaa Ballon d'Or kwa mara ya sita awezi
No comments:
Post a Comment