Umewahi kusikia kauli hizi? " Mume wangu hatosheki
kitandani.." "..Sidhani kufanya mapenzi ndio liwe jambo la msingi
lakini huyu mwanaume kaa! Basi tu kila siku mpaka kero.."
Bila shaka ni kilio cha wanawake wachache walioamua kusema.
Hivi kweli ni mara ngapi au kiasi gani tuseme inatosha? Je wanaume wanafanya
makusudi? Je kuna uwezekano wakabadilika?
Katika mapenzi, suala la kumtaka mwenza kimapenzi hutegemea
sababu nyingi, chache ni uwezo wa kiafya, utayari wa kihisia, usalama wa kazini
na mengineyo. Japokuwa jinsia zote huwa na kiu ya mapenzi lakini wanaume huwa
ni zaidi.
Daktari David Reuben anasema kuwa ".. Wanaume wengi
huzungukia ktk mzunguko wa saa 48 yaani huhitaji kukutana kimwili kila baada ya
saa 48 ili wawe ktk hali njema ya kimwili na kiakili..."
Nae Daktari na mwandishi Dr Herbert Miles anasema "..
Mwanaume mwenye afya njema mbegu hujaa kila baada ya saa 42 hadi 78 na
kuzalisha nguvu kali inayohitaji zitolewe.."
....
Pia mwanasayansi Alan Frome anasema kuwa '.. Wanaume
wanaonekana kuwa na njaa ya kukutana kimwili kwa sababu ya maumbile ambapo
prostate gland ina kifuko kidogo kitunzacho mbegu, na kijaapo, mwanaume
huhitaji kuzitoa, presha huzidi zaidi na zikitoka hurudi ktk hali yake ya
kawaida.."
UPANDE WA WANAWAKE
Wanawake hutofautiana kabisaa na wanaume hali kadhalika na
wao kwa wao. Kwa mujibu wa utafiti wa Johnson Masters 2010, kwa wastani 20-25%
ya wanawake huwa na mtazamo hasi au vuguvugu ktk kuhitaji kukutana kimwili.
2% hawajali kabisa kuhusu kukutana kimwili.
25% zaidi huhitaji sana, husaka kukutana kimwili na
huanzisha hitaji hili hata kabla ya mwanaume kusema.
50% iliyobaki huwa na uhitaji wa wastani tu.
Ifahamike pia hasa kwa wanaume kuwa, hali ya mwanamke
hubadilika sana ktk kuhitaji tendo la ndoa ktk kipindi cha mzunguko wa siku
zake.
Lakini mwanamke anapofikia miaka 40+ hitaji la kukutana
kimwili hulingana karibu na lile la mwanaume
NINI KIFANYIKE
Wanaume ambao hawajaoa wanapaswa wajikite sana ktk shughuli za
uzalishaji mali zinazochosha mwili au mazoezi na kuepuka mambo yanayochochea
hisia za mapenzi hapo wataishinda saa ya 48, Walio ktk ndoa wawe na utaratibu
unaokubaliana na hali ya mwanamke na wajenge mazoea ya kufanya romansi sana ili
kuendana na mabadiliko ya mwanaume na kuepusha utumwa wa ngono ndani ya ndoa au
kukimbilia nje ya ndoa hali inayoleta magonjwa, kutelekeza familia na mengineyo
yasiyoleta furaha ya familia.
No comments:
Post a Comment