UKIONA DALILI HIZI UJUE HAKUNA MAPENZI HAPO - waleo blog

Breaking

Wednesday 18 December 2019

UKIONA DALILI HIZI UJUE HAKUNA MAPENZI HAPO

#MAHUSIANO

1 : Hataki kuambatana wewe katika matembezi na ikitokea anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au pengine kutembea nawe kwa umbali.

2 : Anapata kigugumizi kukutambulisha kwa rafiki, ndugu na inapotokea amebanwa hafikishi ujumbe kwa kiwango timilifu.

3 : Haoneshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleao, kwake ni kufuja mali na anapokosa kupewa pesa ni mwepesi kulalamika na wakati mwingine kununa kabisa.

4 : Anaahirisha mara kwa mara kukutana na wewe tena bila kukueleza sababu za msingi au kukutungia uongo wa dhahili na kuusisitiza bila kuona aibu.

5 : Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanaume amtakaye sifa zake zinakuwa hayalingani na wewe. Anaweza kukuambia napenda kuishi na mwanaume mwenye gari au mwenye mwili mkubwa, sifa ambazo wewe huna!.

6 : Hacheki kwa furaha hata kama ukimchekesha haoneshi furaha ya moyoni. Tena mara nyingine anakuwa mkimya na mshawishi mkubwa wa kuachana kutoka kwenye matembezi yenu ya jioni. “Utasikia  aaah!!, mi nimechoka narudi nyumbani”


7 : Anajaribu kukuunganisha na wanawake wengine na haoni vibaya anaposikia unamfukuzia mwingine badala yake anakutia moyo wa kuendelea na usaliti wako. Hana wivu kabisa.

8 : Hajuti anapokukosea, mwepesi wa kujitenga, kutokuzungumza nawe na mwingi wa kukusukumia makosa hata kama yeye ndiye aliyekukosea.

9 : Msambazaji wa habari za udhaifu wako na mtu asiyekusifia mbele za wenzake. Si balozi mwema kwa familia yake, haishi kukuponda mbele ya wazazi na ndugu zake.

10 : Mwepesi wa kupokea na si wa kutoa mmiliki wa mali zako na mkumbatiaji wa mali zake. Msiri wa mipango yake na mtu anayependa kujua zaidi ya kwako kuliko wewe kujua yake.

11: Hathamini uwepo wako na anakuchukulia kama mtu wa akiba. Hakumiss unapokuwa haupo, hahisi upweke wala hakukumbuki unapokuwa mbali naye.

12 : Hakutii moyo unaposhindwa na mara nyingine hahuzuniki unapokuwa una shida,. Hachukulii huzuni yako kama yake, hakufariji na hakusaidii kutatua kilichokwama kwako.

13 : Mhamasishaji wa uasi hasa wa watoto na ndugu, anaweza kuchochea hisia za jamii ikuone mbaya, kukudharau na wakati mwingine ikutenge na ni mwenezaji wa sifa zako mbaya.

14 : Hakupi kipaumbele katika maamuzi, anajiona yeye ndiye wa kwanza na wewe ni mtu wa kufuata hata unapopinga hasitishi dhamira yake ya kutenda.

15 : Humsisimui katika mambo ya faragha, anakuchukulia kama ndugu yake.


16 : Hakuhudumii tendo la ndoa mpaka siku amependa mwenyewe. Ni mwingi wa sababu za kuchoka kusingizia ugonjwa na mwenye kuhisi kero ya kucheza nawe mchezo wa kikubwa.

17 : Hazungumzii maendeleo yenu, mwepesi wa kushawishi vilivyopatikana viuzwe ili atimize hitaji lake. “Usishangae ukasikia, niuze simu yangu niende kuwaona wazazi, maana kuna sherehe ya mototo huko!”

18 : Hataki kuambiwa ukweli na anapotokea akaambiwa anajitetea kwa kumtaja mwanaume mwingine. “Mbona Saad fundi bomba (si jina halisi) anamfanyia hivi, hamfanyii hivi mkewe”

19 : Hasamehe na kusahau. Kosa la mwaka juzi analijengea hoja.

20 : Mwepesi wa kutoa kauli za kutengana na asiyeogopa kuachwa. “Kama vipi kila mtu akae kivyake maana naona unaniboa tu, unadhani nitashindwa kuishi bila wewe”



No comments:

Post a Comment

Pages