#MAISHA
Nimezipenda hizi nasaha. Naamini na nyinyi wenzangu hamtakosa japo machache ya kujifunza:-1. Epuka hasira za ovyo na kila mtu
Kuwa msikivu kabla ya kukimbilia maamuzi (elewa kuwa ukiwa na hasira huwezi kupata suluhu ya jambo)
2.Usiwatendee wengine ubaya
Ipo siku ubaya wako kwa wengine utakurejea kama sio kuwarejea watu wa kizazi chako
3. Usichukue maamuzi kabla ya kutafiti
Mtuhumu mtu lakini mpe muda wa kumsikiliza, usimshambulie mtu kwa maneno makali bila kuujua ukweli, ukijua ukweli nafsi inaweza kukusuta.
4. Mchukulie kila mwanadamu ni mkosaji
Tambua kuwa hata wewe unawakosea sana wengine na wanakuvumilia. Hivyo usiwe mwepesi wa kuwaadhibu wenzio kwa ubaya
5. Usipande mbegu za chuki na ubaya
Usiadhani itakuacha salama chuki hukua kama mti utambaao, ukiipanda ndani ya jamii yako, haitatoka kwako na inaweza kutafuna kizazi chako ukajutia.
6. Tambua kuwa yule unayeishi nae ni mwanadamu kama wewe
Mpe heshima na mwonyeshee upendo hata kama huoni anafanana nawe. Maisha ni duara huenda ulikuwa kama yeye au atakuja kuwa kama wewe baadae.
7. Usiwe muongeaji ovyo ovyo na usiye na subira.
Kuongea sana kunapoteza busara.
8. Jiepushe na maisha ya kusukumwa na wengine
Yaani kufanya jambo usilojua manufaa yake. Jifunze kujitegemea kiakili. Sio kila unayemdhania rafiki moyoni mwake yupo pamoja nawe, na ukashirikiana nae, wengi wa marafiki zetu hututumia sana kuliko tunavyoweza kuwatumia wao.
9. Usipende sana kugombana na watu kwa njia ya maongezi yanayodumu kama vile
Ujumbe wa maandishi, mawasiliano ya simu au ujumbe wa maneno (SMS). Kumbuka kuwa maneno yanaishi kuliko ugomvi au uadui, ipo siku yatakurudi na utajiona mpumbavu na kukosa pa kujificha. Jifunze kusubiri
.
10.Usifumbue mdomo wako kutamka ubaya au kunyanyua kidole chako kuandika ubaya juu ya mwenzio bila kujiuliza mara mbili moyoni mwako hatima ya unachokitoa kwa mwingine.
10. Jishushe na jifunze kusikiliza wengine
Wakati wa mazungumzo ili uweze kujifunza kabla ya kukurupuka kujibu, usikivu ni kipimo cha busara, mtu anayekurupuka kujibu jibu kila anachosikia hawezi kuwa kiongozi, Mume au Mke mwema kwani mara nyingi atapotoka tu
11. Usitunze hasira nyingi moyoni kwani hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu. Jitahidi pia kuepuka kuwa na hasira mara kwa mara na zisizo na maana. Elewa kuwa hasira zisizo maana hukupunguzia maisha na kukupa maumivu wewe mwenyewe kuliko yule uliyemfanyia hasira, utakufa kwa magonjwa kabla ya wakati ufaao
12. Thamani yako inategenezwa na watu wengine,
Wewe kama ni mtoto, mheshimu sana mzazi wako na kama umeoa au kuolewa, heshimu wazazi na familia ya mke au mumeo kwa kuwa bila wao, usingekuwa hivyo ulivyo leo unajivunia ndoa njema, kwa kuwa yupo mtu alimzaa huyo mwenzio. Mheshimu kwa lolote liwe jema au baya, utalipwa kwa wakati ufaao
13. Usijibizane na mtu usiyemjua au ambaye hawezi kukupunguzia kitu katika maisha yako. Tambua kuwa unapunguza sehemu kubwa ya maisha yako kwa kutafuta magomvi na mtu wa mbali nawe.
14. Kumbuka asili yako
kumbuka upo hapo kwa kuwa kuna mahali ulitoka, maisha yanabadilika, usidharau pale ulipokuwa zamani kwa kuwa ndipo palipokufanya leo uwe hapo.
15. Subiri, sikiliza, elekeza, vumilia
Elewa sio kila mtu ana uelewa kama wako. Jitahidi kuwa mvumilivu katika kila jambo, usiinuke kuwafokea au kuwakaripia wengine kwa jambo ambalo pengine nao wanahitaji muda kueleweshwa ili walifanye vyema. Kumbuka sana, kuna wakati nawe ulikuwa huelewi kabisa lakini wapo wenzio walikuvumilia, wakakuelekeza njia njema, kufokea wengine mara kwa mara sio njia njema ya kuwafundisha bali ni kuwaweka mbali nawe.
#SHARE,LIKE,COMMENT AND FOLLOW US
No comments:
Post a Comment