MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOANZISHA MRADI WA UZALISHAJI - waleo blog

Breaking

Thursday 21 November 2019

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOANZISHA MRADI WA UZALISHAJI

#UJASIRIAMALI
Image result for picha mtu anaweza
Miaka ya karibuni kumekuwepo na kampeni kubwa ya maendeleo ya kilimo inayofanywa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa sekta hii kuwahamasisha wakulima kukifanya kilimo chao kama shughuli kamili ya kuwaingizia kipato. Wale ambao walikubali kubadilika na kuzingatia kanuni kwa kuajili watu wenye busara, weledi na maarifa ya usimamiaji wa shughuli hizi hivi sasa wanafaidika nazo, kwani wanapata pesa za kutosha zinazoingia mifukoni mwao kila kukicha na wameweza kuziba mianya yote ambayo hupelekea upotevu wa pesa zao.
Faida kama hizo hazipatikani kwa urahisi. Kuweza kutambua wazo linalofaa kwa biashara pia haitoshi, huu unakuwa ni mwanzo tu. Lazima pesa kwanza ipatikane kama mtaji wa kuendeshea shughuli za biashara husika ili mwisho wa siku zikuingizie ziada ya pesa ulizowekeza (faida) kutokana na mauzo ya biadhaa zilizozalishwa au huduma uliyoitoa kwa wateja. Hapa ndipo suala la kuwa na mipango thabiti ya biashara linapokuja endelea…

NINI MIPANGO YA BIASHARA?
Pale unapoomba mkopo kutoka kwa taasisi husika za kutoa mikopo ambapo mara nyingi huwa ni benki, taasisi zingine za fedha dhahiri kwanza watapenda kujua mpango wako wa biashara (Business plan). Mpango huu utaonyesha malengo ya biashara inayokusudia kuifanya, kwa nini unafi kiri malengo haya yanaweza kufi kiwa, na pia itabainisha mikakati mbalimbali ya kuyafi kia malengo hayo.
Mipango yote ya kuanzisha biashara lazima iwe kwenye nyaraka zilizoandaliwa vilivyo ili kushawishi taasisi za fedha kukuazima fedha.
Bahati mbaya wakulima wengi hawana ufahamu wa kutosha kwenye eneo hili la kupanga biashara za kilimo. Na itabidi ieleweke kwamba bila ya kuwa na nyaraka (documents) itakuwa ni vigumu kumshawishi mtu binafsi au taasisi za kifedha kukuazima fedha zao ili uwekeze kwenye biashara unayotaka kuifanya.
Mpango wa biashara utatofautiana na ukubwa wa biashara, aina za teknolojia zitakazotumika na kwa nani hiyo mipango inakusudiwa. Kwa ujumla mpango wa biashara utatarajiwa kujumuisha vifuatavyo:
• Muhstari wa utendaji mzima (Executive summary): Lengo la sehemu hii ni kutoa picha kamili ya uwekezaji husika. Hujumuisha uanishaji wa biashara yenyewe, mazao au bidhaa, huduma na muhtasari wa uchambuzi wa mikakati ya masoko na mipango ya pesa. Sehemu hii lazima ianishwe kwa upana ili kubainisha mawazo yako na picha kamili ya biashara unayotaka kuifanya. Lazima ubainishe kwa kadiri inavyowezekana dhumuni hasa la pesa unazozitafuta. Na mwisho wa muhtasari huu wa utendaji mzima lazima kuwe na maelezo ya kuvutia ili kumshawishi msomaji wako kwamba biashara hiyo itakuwa na faida. Muda muafaka wa kuandika muhtasari ni baada ya kutayarisha azimio (Proposal) na uingize mwanzoni mwa mpango wako wa biashara.
• Wazo la shughuli husika (Bussness idea): Hii itatoa taarifa kuhusu aina ya bidhaa, zao au huduma utakayouza au kuitoa kwa wateja.
• Mipango ya soko: Hii itajumuisha kila kitu ambacho utakachokifanya kuonyesha nani wateja wako, nini wanahitaji au kukitaka na namna gani ya kuwafi kia. Sehemu hii itatoa maelezo ya bidhaa yako au huduma kwa maelezo ya kina. Pia itajumuisha maelezo ya kiasi cha bei utakayotoza, sehemu ambapo biashara yako itakuwa ikifanyika na njia za usambazaji wa bidhaa au huduma husika utakazotumia na namna ambavyo utainadi (Promote) biashara yako.
• Muundo wa biashara: Hii itaelezea hadhi ya kisheria ya biashara yako, muundo uliochagua kutegemeana na faida na hasara ambazo kila muundo unao. Machaguo ya aina ya umiliki, ubia, au kampuni yenye hisa kikomo au ushirika. Pia katika kifungu hiki itabidi ujumuishe ubainishaji wa namna gani umefi kiria kupitia matakwa ya kisheria na namna ulivyoyatumika katika mchakato mzima wa uanzishwaji.
Usimamizi: Kifungu hiki kinajibu swali kuhusu aina gani ya ujuzi na weledi wafanyakazi wako wanahitaji kuwa nayo, wangapi utawahitaji na namna ujuzi na weledi wao utakavyosaidia kufi kia malengo ya biashara uliyoyakusudia.
Mipango ya fedha: Utahitaji kuwa na bajeti yakinifu ya biashara yako. Hivyo kifungu hiki itakusaidia kuwa na mipango thabiti kwa faida ya biashara yako na mtiririko mzima wa pesa ya biashara yako hii mpya. Kwa maana pesa inayoingia (mapato) na pesa inayotoka (matumizi). Mara utapokuwa umeandaa bajeti yako utaweza kutumia taarifa hizi kujua kiasi cha pesa utakachohitaji kuanzisha biashara yako. Hii hujulikana kama mtaji wa kuanzia (Start up capital). Itabidi uoneshe chanzo cha mtaji huu wa kuanzia biashara kwa maana ni chanzo kipi kitachangia kiasi hiki na asilimia ngapi ya pesa inayohitajika

DONDOO ZA KUZINGATIA:
• Mtaji: Hii hujulikana kama pesa ya mwanzo ambazo huwekezwa kwenye mradi wa uzalishaji ni vema mkulima akatambua ni chanzo kipi na kwa asilimia ngapi kitachangia kwenye mtaji.

ZINGATIA:
• Mpango wa biashara: Huu ni mwongozo wa kukusaidia kuendesha mradi wako. Hivyo ni vizuri kuwa na mpango unaofaa kukusaidia
kuendesha mradi wako. Huu una msaada mkubwa kwa kuwa ni msingi mmojawapo wa biashara. Kuandaa mpango mzima wa namna ya kuendesha biashara yako hakukuhakikishii mafanikio kwa asilimia mia moja lakini ni njia ya maana kukupunguzia uwezekano wa kuanguka kwa mradi wako. Na ndiyo dira ya uendeshaji wa shughuli zako

JIULIZE:
Kuna maswali muhimu ambayo kila mmoja wetu anapasa kujiuliza kabla ya kuanza miradi ya uzalishaji nayo ni:
• Je, nina muda wa kutosha kusimamia mradi wangu mpya?
• Je, idadi ya kazi zilizopo kwenye mradi husika zinashahabiana na kiasi cha muda nilio nao katika mwaka ambao nitalazimika kufanya kazi?
• Je, mradi wangu mpya utaweza kusaidia utendaji wa shughuli zangu za sasa?
• Je, nina malengo niliyoyaandikisha ambayo yanaelezea matokeo ninayotarajia?
• Je, nina ujuzi na weledi wa kutosha wa kuendesha shughuli za mradi husika?
• Ningependa kusimamia watu iwapo nitahitaji wafanyakazi?
• Nilishawahi kusimamia mradi wowote wa uzalishaji kabla?
• Binafsi Nina nguvu za kutosha za kuendesha mradi?
• Nina ndugu wengine kwenye familia wa kuweza kunisaidia
• Najali kama kuhusu nini majirani zangu wanafi kiri kuhusu mradi wangu?
• Na kwa nini nahitaji kuwa na mradi huu?

Share this:

Share

No comments:

Post a Comment

Pages