Mahindi ni zao muhimu linalolimwa katika maeneo ya kitropiki. Pia zao hili hulimwa katika udongo wenye uchachu pH 6-6.5. Lakini pia hustawi zaidi kwenye maeneo yenye mwinuko.
KANUNI YA KWANZA : KUTAYARISHA SHAMBA MAPEMA
i Tayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita.
ii Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba na usiosimamisha maji.
iii Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.
1. Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa kutumia jembe lolote.
2. Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.
3. Hupunguza magugu.
4. Hupunguza wadudu waharibifu.
KANUNI YA PILI : KUJUA WAKATI WA KUPANDA MBEGU SHAMBANI
Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua haitabiriki, Kama mvua
hunyesha nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo
inaonyesha tahere za kupanda zao la mahindi katika eneo lako.
1. Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni.
2. Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati hadi Februari katikati
3. Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni
4. Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari mwanzoni.
Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao
mengi ni mkubwa. Kwa mashamba makubwa makubwa sana wakati wa kupanda uwe
wiki moja kabla ya mvua kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya
mvua.
Isiwe mapema zaidi kwani mbegu zitaharibiwa na joto katika udongo, wadudu, panya, ndege na wanyama wengineo.
FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA
i Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
ii Magonjwa kama yale ya ya majani hayatatokea au yatakuwa kidogo.
iii Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.
KANUNI YA TATU : KUCHAGUA MBEGU BORA
Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.
i Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
ii Huzaa mazao mengi.
iii Hustahimili magonjwa.
AINA ZA MBEGU
i Mbegu aina ya chotara(hybrid)
ii Aina ya ndugu moja(synthetic)
iii Mbegu aina ya composite
Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika misingi ya
kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80 au tani 5.5 – 7.5 kwa hekta
moja au kumi kwa hekari.
MAPENDEKEZO YA MBEGU ZA KUPANDA
Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa SIDCO
,PANNAR, CHOTARA, kutoka KENYA n.k Ni vyema kufuata ushauriwa wataalamu
wa kilimo
KANUNI YA NNE : KUPANDA
Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani ikizidi
a) Mazao hupungua.
b) Mmea huangushwa na upepo
c) Mabua mengi hayazai.
Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababishwa mavuno kupungua jambo la kufanya ni kupanda mbegu
katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na wataalamu.
KIASI CHA KUPANDA
a) Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali (sumu)
b) Kiasi cha kilo 20 (ishirini) za mbegu kinatosha kupanda hekari moja. (Hii hutegemea na aina ya mbegu)
NAFASI ZA KUPANDA
75cm x 30cm
75cm x 60cm
90cm x 25cm
90cm x 50cm
KANUNI YA TANO : KUTUMIA MBOLEA
Mahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwa mbolea pamoja na
matunzo mengine ya kilimo bora. Ukipanda mbegu bora bila kutumia mbolea
ni kazi bure.
KUNA AINA MBILI KUU ZA MBOLEA
1. Mbolea za asili mfano; samadi, mboji na majani mabichi, mbolea
hizi hua na virutubisho vya kutosha ambavyo havijulikani vipo kwa kipimo
kiasi gani
2. Mbolea za viwandani, hizi hua na virutubisho vya kutosha na
vipimo hujulikana, hii inasaidia kujua ni kiasi gani kitumike kwa
kipindi gani.
No comments:
Post a Comment