SAMATTA APEWA MTAA - waleo blog

Breaking

Monday 3 June 2019

SAMATTA APEWA MTAA


 

Samatta ni miongoni mwa wanamichezo wawili ambao wamepewa heshima hiyo hivi karibuni, mwingine ni nyota wa zamani wa riadha, Filbert Bayi

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amepewa heshima ya jina lake kuitwa moja ya mitaa jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wamelazimika kumpa heshima hiyo Samatta kutokana na heshima anayoipa nchi kwenye soka.


"Tulimuita na kuzungumza naye, amepokea taarifa hizi kwa furaha na mchakato kwa ajili ya kuzindua mtaa huo inaendelea," alisema Makonda.

Alisema mtaa huo utakuwa manispaa ya Temeke na utazinduliwa baada ya Taifa Stars kurejea kutoka katika Afcon.  


No comments:

Post a Comment

Pages