Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli amesema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakitengeneza vitabu vya
hesabu ili kukwepa kupeleka kodi kubwa ya ongezeko ya thamani Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA).
Amesema linapofika suala la kuwasilisha asilimia 18 ya VAT
wengi wamekuwa wakibaki nayo kama mtaji badala ya kuipeleka serikalini huku
akibainisha wamekuwa wakitengeneza vitabu tofauti.
“Kimoja ni cha benki chenye mahesabu ya kweli yenye faida na
kitabu kingine ni cha TRA. Kwa kawaida kile kinachopelekwa benki kinakuwa cha
kweli lakini kinachoenda TRA ni kidogo wakati mwingine kinaonyesha hasara,”
amesema Rais Magufuli leo katika mkutano kati yake na wawakilishi wa wafanyabiashara
kutoka wilaya zote nchini unaojadili changamoto wanazokutana nazo na
kuzitafutia majibu.
“Nataka nitoe mfano wa kampuni tatu, moja ya kampuni (Jina
linahifadhiwa) ina vitabu vitatu na fedha zake ni hatari ukiangalia, nina
uhakika huyo mfanyabiashara ataenda akairudishe hiyo hela iliyokuwa inatakiwa,”
amesema Rais Magufuli .
“Kampuni nyingine namba mbili (Jina linahifadhiwa) taarifa
ya benki inaoyesha mwaka 2017 inaonyesha faida ilikuwa Sh958 milioni lakini
iliyopelekwa TRA ni Sh20 milioni kwenye kitabu cha pili, kampuni namba tatu
mwaka 2017 taarifa ya benki inaoyesha faida ilikuwa Sh501 milioni lakini TRA
iliambiwa kuwa imepata faida ya Sh72 milioni.”
No comments:
Post a Comment