Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi ya kuzungumza na
mwanamke au msichana. Kwa njia hii wanaume wengi wanaishi maisha ya bila
kumvutia mwanamke yeyote.
Hapa kunanjia 15 utakazozitumia wewe mwanaume ili
kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo ;
1. Wakati uungumza nae, jaribu kuzungumzia “hisia” kama
vile kumbu kumbu yako ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada
hii ya mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla
.
2. Wanawake huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa
kuwamiliki na kuwaongoza. Wakati unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu
na kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza kufikiri kuwa nini ulichokuwa
ukizungumzia.
3. Kuwa makini wakati unapokuwa ukizungumza nae huku
akikupatia majibu yasiyo na hisia zozote za mapenzi. Hapo utajua kunakitu,
hivyo kama kwa bahati mbaya uko nae karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze
pembeni wakati ukiwa unaendelea kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona
hayuko sawa katika utoaji majibu.. kwa kawaida atakuonyesha ishara, hivyo kuwa
nazo makini.
4. Kumbuka hii kauli mbiu “Ucheshi/vituko si mapenzi”.
Wanawake huvutiwa sana na wanaume wanaoweza kuwafanya wawe na furaha muda wote.
Usijikite zaidi katika kufanya utani unaopita kiasi na kusahau ulichokuwa
unaongea. Bali jikite zaidi katika mambo yanayomfanya ajisikie kuwa na msisimko
na starehe wakati ukonae.
5. Zama katika undani wa mazungumzo baina yako na yeye.
Mwanamke huendana na mwanaume asiyekuwa muoga wa kuzungumzia mambo binafsi kwa
ukaribu
.
6. Wanawake wengi hupenda kujua maoni yako kuhusiana na
jinsi unavyomuona. Mwambie vitu unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu kuwa
makini ili usitamke vitu vingine vitakavyo msababishia apoteze furaha
.
7. Epuka kumpa ofa nyingi mwanamke, mwanamke huwa na mashaka
na mwanaume anayempatia vitu vingi kwa wakati mmoja ama kila mara. Kwasababu
atafikiri vitu unavyompatia ni kutaka kumvutia tu ili umpate kiurahisi. Kitu
ambacho baadae kitaleta madhara makubwa
.
8. Kama unahitaji kujua njia nzuri ya kuweza kuongea na
mwanamke au msichana bila kumfanya asikudharau au kuboreka, basi usitumie njia
ya kumuuliza maswali mengi katika mazungumzo yenu. Bali jaribu kueleza mawazo
yako kuhusu vitu flani.
9. Kumbuka kauli juu ya kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza
“wewe umekulia wapi?”, uliza “unaonekana kama hujakulia maeneo haya!” Hii
itakusaidia wewe kufanya uchunguzi juu yake bila yeye kujua.
10. Usifiche utambulisho wako – zungumza vitu kutoka katika
hisia zako, onyesha uhalisia wako katika kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu
yeyote.
Njia bora ya kufikiria jinsi ya kuzungumza na mwanamke, ni
kutambua njia sahihi ya mazungumzo ya furaha na yakimahaba utakayopenda
kuitumia, isipokuwa usimuige mtu. Kuzungumza na mwanamke sii vigumu bali
nikujua ni vitu gani hasa mwanamke hapendi kuvizungumzia na vitu gani anapenda
kuvisikia. Fuata maelekezo hapo juu utaona matunda yake…kisha rudi toa maoni
yako hapa.
MUHIMU: Maelekezo haya yote yatafanikiwa kwa mwanamke mwenye
kuhitaji mapenzi ya kweli – yani sio kwa wanawake wanaolenga kuchota pesa kwako
na kutokomea. Hivyo kuwa makini sana
No comments:
Post a Comment