#AFYA
Kubemenda
ni lugha inayotumiwa na watu wengi kwa maana ya kuwa “mtoto ameharibiwa afya yake sababu ya wazazi wake” mara nyingi taswira hii ya kudhoofika kwa mtoto huendana na matazamio ya kwamba
mzazi mmoja (mke au mume) ametoka nje ya ndoa na kutembea na mtu tofauti au
mama anayenyonyesha na kubeba
ujauzito mwingine.Kwa kawaida mama mjamzito baada ya kujifungua
huchukua muda upatao kati ya miezi mitatu hadi nane kurudia kwenye mzunguko wake wa hedhi (siku zake) bila
kujali amepasuliwa au amejifungua kawaida,muda huo ambao hapati siku zake ni
vigumu kupata ujauzito mwingine hata kama akikutana na mume.Lakini baada ya
kuanza kuziona siku zake ni wazi kuwa uwezekano wa kukutana na mume na kupata
ujauzito ni mkubwa sana.
Miongozo
ya dini nyingi huelekeza muda wa mume kuweza kukutana na mke wake baada ya
kujifungua,na haikupangii wewe ni lini na muda gani utafanya hivyo au ni namna
gani utajikinga na ujauzito usiotarajia maana hii huwa ni baraka za mungu
kukujalia uzazi.Kwa upande wa tamaduni za jamii zetu ni kuwa mwanamke
baada ya kujifungua huweza kuacha kushiriki shughuli za ndoa (tendo la ndoa)
akiwa pamoja na mwenza wake (mume) au hata kutengana kabisa na mume wake kwa
kipindi fulani kwa ajili ya kulea mtoto aliye zaliwa.
Kwanini mtoto adhohofike kiafya.
Kuachishwa kunyonya mapema kabla ya mwili wa
mtoto haujazoea kutegemea vyakula kujijenga kiafya,hii hupelekea uwezo wa
kukabiliana na magonjwa ni mdogo hivyo kuugua mara kwa mara na kupelekea kuzorota kiafya.Hatua hii
mara nyingi huchukuliwa kutokana na kubeba ujauzito mwingine kabla ya mtoto aliyetangulia
hajamaliza kunyonya.lakini hilo siyo tatizo kwani hakuna uhusiano wowote ambao
unaweza kumdhuru mtoto akinyonya maziwa ya mama yake mjamzito.Kumwachisha
kunyonya ndio tatizo linalodhoofisha mtoto na siyo mimba aliyobeba mama.
Uchafu wa wazazi (mke na mume) kutozingatia mazingira na wakati mzuri wa
kukaa faragha wakati mtoto akiwa mbali nao.Tunaposema uchafu wa wazazi ni
kwamba wazazi wanashiriki tendo la ndoa na lakini bila kujali kuoga kabla
ya kunyonyesha au kumshika mtoto.Faragha kunakuwa na mipapaso,mihemko,kuingiliana
kimwili,kulambana,kunyonyana au kuchezeana maeneo mbalimbali ambayo hurudiwa
mara kwa mara hivyo huweza kusafirisha uchafu wa sehemu za siri (baada
ya kuingiliana kimwili)kuja hadi kwenye mikono,matiti n.k kwa namna hii mtoto akinyonyeshwa
kabla ya kujisafisha basi atakuwa anakula uchafu na matokeo yake kuharisha na
mengineyo.muhimu kuoga kabla ya
kunyonyesha na tafuta muda wa kukaa faragha mtoto akiwa amelala au yupo maeneo
ambayo huweza kukaa muda mrefu bila kulilia kunyonya.
Miiko na tamaduni mbaya zinazokandamiza
upatikanaji wa chakula bora kwa mtoto hasa akiwa bado mdogo,kipindi cha utoto
kunahitajika chakula chenye virutubishi vingi ili kukuza afya ya mtoto.
Magonjwa ya utapiamlo na mazingira machafu ya
kuandalia chakula, hivyo vimelea vya magonjwa huweza kumshambulia mtoto kwa
urahisi kutokana na kwamba kinga zake za mwili ni ndogo sana ukilinganisha na
kinga za mtu mzima.
Tujitahidi usafi kina baba na kina mama ili
motto awe na afya bora.
Share na wengine waelimike na wakumbuke.
No comments:
Post a Comment