ASILI YA LIMAO NA FAIDAZAKE - waleo blog

Breaking

Sunday, 23 February 2020

ASILI YA LIMAO NA FAIDAZAKE


#TIBA LISHE

Limao ni tunda la mlimao. Pamoja na chungwadansibalungindimu ni mojawapo kati ya matunda chungwa.
Rangi ya tunda lililoiva na kukomaa ni  njano-kijani. Maji yake yana asidi nyingi na ladha yake ni chungu. Matumizi yake ni katika upishi hasa na tunda haliliwi moja kwa moja kutokana na uchungu mkali. Maji yake hutumiwa kwa ajili ya vinywaji ama kama kiungo pamoja na maji ya matunda mengine au mara nyingi kwa kuongeza sukari na maji.
Limao lina vitamini C nyingi ndani yake na kiasi kidogo kinatosheleza mahitaji ya kibinadamu. Sifa hii ilitambuliwa wakati mabaharia kwenye jahazi walipata ugonjwa wa kiseyeseye uliokuwa na balaa kwa safari za kwanza zilizovuka bahari za Atlantiki na Pasifiki wakati wa upanuzi wa Wareno, Wahispania na Waingereza kuanzia karne ya 16. Hapa limao zilitambuliwa kuwa dawa lililozuia ugonjwa huu kutokana na kiasi chacke cha vitamini C.
Limau/limao ni tunda, mti mdogo ambao daima kijani, cirtrus limon, asili yake Asia na pia ni jina la mmea wake. Tunda la limao hutumiwa kwa makusudi ya mapishi na mengine yasiyo ya mapishi hasa kwa majimaji yake, japo nyama zake na pia maganda yake hutumika hasa wakati wa kupika na kuoka. Majimaji ya limao ni asilimia 5 asidi sitriki asidi ya matunda jamii ya machungwa  ambayo hulipa limao radha ya uchachu, na ph ya 2 mpaka 3, hii hufanya kujipatia asidi ya gharama nafuu kwa ajili ya mafunzo ya kielimu. Kutokana na radha yake ya uchachu, vinywaji vingi na peremende vilivyokolezwa na radha ya limao vinapatikana.

Asili kabisa ya limao bado haijulikani, japo inaaminika kuwa mimea ya kwanza ilipatikana huko India, Kaskazini mwa Bama na China. Huko Kusini na kusini mashariki mwa Asia yalifahamika kwa uwezo wake wa matibabu na ukatumika sana kama dawa kwa sumu mbalimbali. Baadae ukafahamika huko Persie na kasha Misri na Iraki mnamo 700bk. Mlimao ulisambaa sana miongoni mwa jamii ya Uarabu na Ukanda wa Mediteraniani kati ya 1000 na 1150 BK. Malimao yaliingia ulaya baada ya karne ya kwanza BK, wakati wa utawala wa Roma.
 Hata hiyo mmea huu ulikua haulimwi sana. kilimo cha limao kilianza karne ya kumi na tano huko Genoa. Baadae yalifika mpaka  America mwaka 1493 wakati ambapo Cliristopher Columbus alichukua mbegu za limao na kwenda nazo Hispania wakati wa safari zake. Kutoka Hispania malimao yalisambaa sana na yalikuwa yakitumika hasa kwa mapambo na dawa na miaka ya 1700 na 1800, malimao yalikuzwa sana huko Fhorida na Calfonia baada ya malimao kuanza kutumika kupikia na kama viungo vya kuongeza ladha. Mnamo 1747 utafiti wa James Lind ulithibitisha kwamba unavitamini C kutoka kwenye limao, yaliweza kuwatibu baharia ugonjwa wa ngozi wa kiseyeye.
Malimao yanafahamika kama msaada mkubwa wa umengenywaji wa chakula, mchanganyiko wa asali nyeusi na makapi huwa kwa kiwango kizuri katika kusafisha oganiza umegaji wa chakula. Virutubisho vingine hujumuisha maji -89%, asidi ya sitriki -5%, makapi -2.8%, sukari – 2.5%, mafuta – pungufu ya 0.3%, protini – pungufu ya 7%, vitamin C, na madini kadhaa kama vile selenium, zinc manganese, na shaba. Vitamin C katika limao hutofautina. Hutegemea na ukubwa na ukomavu, kuiva  na aina ya sehemu inayoliwa kula limao lililokomaa huwezesha mtu kupata 10,000% ya vitamin c. Zingatia kuwa ni lile ganda la ndani jeupe la ndani ya limao, linalokuwa na kiasi kikubwa cha vitamin c kwa ujazo wake kuliko chakula kingine chochote, uchunguzi unaonyesha, sehemu ile nyeupe kuwa na mara 8 mpaka 11 zaidi ya vitamin c kuliko chupa ya dawa ya vitamin c kutoka hospitali.

Malimao hutumika kutengenezea shamlati na mapambo mezani kwa vinywaji. Magada ya limao pia yanamatumizi mengi. Vinywaji vingi soda, chai na maji. Mara nyingi huandaliwa na kipande cha limao kwenye bilauri au hata kwenye pindo ya chombo husika. Samaki huwekwa maji ya limao kuondoa shombo. Hapo asidi ya limao hubadilisha amaibni, kemikali iliyo kwenye samaki kuwa chumvi za amoniamu, pia hutumika kulainisha nyama na tena kunyunyizia kwenye nyama kabla ya kupika, japo haiui vijidudu. Matumizi mengine, malimao hutumika kutengeneza asidi ya Sitriki, kabla ya njia ya kuchachusha haijafahamika. Hutumika kusafishia vyombo na baadhi ya vitu hasa, hasa kwa ugumu wake ya kuondoa mafuta na madoa.Hutumika kuua bacteria sababu ya kiwango chake kidogo cha pH, majimaji ya limao pia hutumika kusafishia vyombo vya shombo.

Hilo ndio tunda la limao..Kazi kwako kuyapanda kwa wingi.
Sambaza na wengine wapate faida.

No comments:

Post a Comment

Pages