Rais wa Tanzania, John Magufuli amemwagiza Mkurugenzi Mkuu
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwakamata watumishi
watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuwapeleka mahakamani.
Watumishi hao wanatuhumiwa kukamata mizigo ya mfanyabiashara
tangu mwaka 2017 bila sababu wakitaka rushwa.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo June 7, 2019 wakati
alipokutana na wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini Ikulu jijini Dar es
Salaam na kuzungumza nao ambapo wamemueleza changamoto zao.
Kuhusu sakata hilo Rais Magufuli amemtaka Kamshna wa TRA
kuwasimamisha kazi watumishi hao. Sambamba na hilo, Rais ameagiza TRA kumlipa
fidia mfanyabiashara huyo ambaye mzigo wake ulishikiliwa kwa miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment